Serikali yaokoa mabilioni ya wagonjwa kutibiwa nje kupitia JKCI


Serikali imefanikiwa kuokoa kiasi kikubwa cha fedha zilizokuwa zinatumika kupeleka wagonjwa wa moyo nje ya nchi kwa ajili ya upasuaji tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa JKCI,  Dk. Naiz Majani, amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam leo Jumatano Desemba 19.
Dk. Majani amesema hadi sasa taasisi hiyo imewafanyia upasuaji wagonjwa wa moyo 1,040 ambapo kati yao, wagonjwa 600 wamefanyiwa operesheni kubwa na 400, upasuaji wa kawaida.
“JKCI  imeweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo zilikua zinatumiwa na serikali kupeleka wagonjwa wa moyo nje ya nchi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji,” amesema Dk. Majani.
Aidha, amesema taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya ‘Save the Children’ wameanzisha mbio za ‘Heart Marathon’ kwa ajili ya kuhamasisha jamii kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Amesema mbio hizo zinatarajia kumalizika Desemba 28 mwaka huu ambazo zitaanzia na kumalizikia katika eneo la Fukwe za Coco zilizopo Manispaa ya Kinondoni.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja