PIGO JINGINE:Dkt. Mashinji na wenzake watatu waswekwa ndani
Dkt. Mashinji na wenzake watatu waswekwa ndani
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vincent
Mashinji na viongozi wengine watatu wa chama hicho wanashikiliwa na
Jeshi la Polisi wilayani Hai, Mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kufanya
mkusanyiko usio halali.
Hayo
yamesemwa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Hai
ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya ambapo amesema kuwa
viongozi hao wamekamatwa mchana kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko
usiokuwa halali.
“Ni
kweli tumemkamata Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Mashinji, katibu wa
Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Basir Lema, mwenyekiti wa halmashauri ya
Hai, Egra Mchomvu na msaidizi wa mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, Irine
Lema kwa kufanya mkusanyiko usio halali,” amesema.
Amesema
kuwa viongozi hao, wamekutwa wakifanya mkusanyiko katika eneo la Boma
bila ya kuwa na kibali jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Aidha,
Sabaya amesema katika wilaya yake ya Hai kwa sasa hataruhusu mikutano
isiyo halali ambayo inalenga kuwapotosha wananchi kuhusu kazi nzuri
ambazo zinafanywa na Rais Dkt. John Magufuli.
Comments