Posts

MAKONDA : NDEGE MPYA YA TANZANIA AIRBUS KUTUA JUMAPILI 23/12/2018

Image

Mwanaharakati Mtanzania mtetezi wa wasichana ashinda tuzo ya UN

Image
Akiwa na umri wa miaka 31, Rebeca Gyumi tayari anaorodha ya mafanikio ambayo mtu yeyote wa umri wake atapenda kujivunia. Amefanikiwa kupinga mfumo wa sheria nchini Tanzania ambako ndiko aliko zaliwa na kukulia, na kushinda uamuzi wa kesi ya ukombozi wa kipekee ulitolewa na mahakama mwaka 2016 ambao umeongeza umri wa kuolewa kutoka miaka 14 hadi 18. Baada ya ushindi huo alianzisha taasisi ambayo imekuwa ikitetea elimu kwa wasichana; ameshinda Tuzo ya Unicef ya malengo ya kimataifa na ametajwa mwanamke bora mwaka 2016 katika Gazeti la New Africa Magazine. Tayari ameshawasili New York ambako amepokea Tuzo ya Haki za Binadamu 2018 iliyotolewa na Umoja wa Mataifa. “Nilikuwa nimeshtuka sana. Nimeshtuka na kushtukizwa bila ya kujua kwamba ninafikiriwa kutunukiwa zawadi hiyo yenye hadhi ya juu,” ameliambia kituo cha habari cha CNN. Gyumi alikuwa mtoto yeye mwenyewe wakati alipoanza kuona uonevu ukifanyika katika mazingira yake. Alikuwa na umri wa miaka 13 wakati baadhi ya...

Wajue wagombea wakuu wa urais DRC

Image
Katika mfululizo wetu wa Makala kuhusu uchaguzi mkuu wa rais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, leo tunapata maelezo kuhusu wasifu wa wagombea wakuu kwenye kiti cha urais. DRC inafanya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge Disemba 23. Mwenzetu Patrick Nduwimana anaangalia pia sera zinazowekwa mbele na wagombea hao. Idadi ya wapiga kura Zaidi ya raia wa congo millioni 46 watajielekeza kwenye vituo vya kura jumapili, kuwachagua wagombea u rais, wabunge kwenye ngazi ya taifa na majimbo. Wagombea kwenye kiti cha u rais wote pamoja ni 21 akiwemo mgombea moja mwanamke. Lakini hapa tunaangazia wasifu wa wagombea wakuu wa tatu ambao ni Emmanuel Ramazani Shadary, Martin Fayulu na Felix Tshisekedi, pamoja pia na sera zao za kisiasa. Ramazani Shadary ​ Emmanuel Shadary: Emmanuel Shadary ni mgombea wa muungano wa vyama tawala (FCC), aliteuliwa na Rais Joseph Kabila ambae haruhusiwi kuwania muhula mwengine kulingana na katiba ya jamhuri ya kidemokrasiya ya congo. ...

Kubenea alivyo mkataa Makonda

Image
Alhamisi , 20th Dec , 2018 Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Saed Kubenea amesema kuwa kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kusema kuwa yeye na Mbunge wa Kibamba John Mnyika walitaka kujiunga na CCM, si kweli. Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Saed Kubenea. Kubenea amesema kuwa hawakuongea vile na Rais bali walikuwa wakizungumza mambo mengine, na Makonda amesema yale ili kuwafurahisha wanachama wa chama cha mapinduzi waliokuwepo kwenye hafla ile. Kubenea amesema kuwa uchaguzi ujao watahakikisha kuwa wanashinda kwa kishindo hadi serikali inayoongozwa na CCM ishangae. " Nataka nimwambie tu RC Makonda kwamba katika uchaguzi unaokuja upinzani tutashinda zaidi kuliko ilivyo kawaida, na ataondoka kwa aibu ", amesema Kubenea. Kubenea ameongeza, " Nchi yetu inajenga matabaka, mtu akionekana ...

WE CAN, WE MUST ,WE WILL:Dkt. Mengi awapongeza Serengeti Boys

Image
Mlezi wa timu ya taifa ya soka ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi,  amewapongeza wachezaji hao kwa ubingwa wa COSAFA walioutwaa nchini Botswana. Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi akipokea kombe la COSAFA kutoka kwa nahodha wa Serengeti Boys Michael Morris. Dkt. Mengi ametoa pongezi hizo leo Desemba 20, 2018 katika hafla ya chakula cha mchana alioyowaandalia vijana hao pamoja na viongozi wa TFF na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Waziri Harrison Mwakyembe. Akiongea katika hafla hiyo Dkt. Mengi amesema, ''nyinyi mlizaliwa washindi na siku zote nalisema hilo, nawashukuru vijana wangu kwa kutekeleza ahadi ya kurudi na kombe hili kama mlezi wenu nimejisikia vizuri sana'', amesema. Katika hafla ya ch...

Mrema atoa siri na mpango wa kurudi CCM

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party TLP na Mwenyekiti wa bodi ya Parole amesema kuwa hawezi kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli kwa kumfuata ndani ya chama chake bali atafanya hivyo akiwa upinzani. Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party TLP, Agustino Mrema na Rais Magufuli Mrema ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika mahojiano maalum na www.eatv.tv ambayo ilitaka kupata maoni yake juu ya hamahama ya waliokuwa wabunge wa vyama vya upinzani ambao walieleza sababu kuu ya kufanya hivyo kuwa ni kumuunga mkono Rais Magufuli. Mrema amesema, " sina sababu ya kurejea CCM, na ningetaka kurudi CCM hakuna wa kunizuia, ila narudi kufanya nini kwa sababu Rais aliniona nikiwa TLP, nirejee CCM kutafuta nini kama kazi nimepata na nawatumikia watanzania ." " Kuhusu kumuunga mkono Rais mimi nilimuunga mkono akiwa ...

Hakuna upungufu wa dawa" - Bohari ya Dawa

Image
Mfumo wa ununuzi wa dawa wa pamoja kati ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Taasisi ya Huduma za Afya ya Aga Khan umeelezwa kwamba utasaidia kupunguza gharama za dawa nchini Tanzania. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji, Lauren Bwanakunu wakati wa kusaini makubaliano ya ubia kati ya taasisi hizo mbili. Amesema kwa kuagiza dawa kwa pamoja itasaidia kupunguza bei na kuwapunguzia mzigo wa gharama Watanzania. Aidha ameongeza kwamba " Mkataba huu utawezesha kuendeleza na kugundua masoko na kuboresha shina la ugavi wa rasilimali pamoja na kuwatambua wauzaji wakuu ". Pamoja na hayo Bwanakunu amesema mpaka sasa hakuna upungufu wa dawa ikiwemo dawa za magonjwa yasiyo ya kuambukiza pamoja na zile za magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu.

Mbunge wa 10 kujiuzulu, arejea bungeni

Image
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza Mgombea wa Ubunge jimbo la Temeke kupitia tiketi ya CCM, Abdallah Mtolea  kuwa Mbunge wa jimbo hilo baada ya kupita bila kupingwa. Abdallah Mtolea, Mbunge mteule wa jimbo la Temeke. Akitangaza ushindi huo Msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi, amesema Mtolea ameshinda kiti hicho cha Ubunge baada ya wagombea wengine kushindwa kutimiza vigezo vya kugombea ikiwemo kukosea kujaza fomu. " Abdallah Mtolea mgombea wa CCM, ameteuliwa kwakuwa ametimiza masharti yote kama kanuni zinavyoelekeza, na kwa mamlaka niliyopewa kwa mujibu wa sheria namtangaza ndugu Mtolea kuwa Mbunge mteule wa jimbo la Temeke ", amesema Mwakabibi. Mtolea alitangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo na kisha kukihama chama chake cha CUF na kujiunga na CCM, ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM), ...

AliKiba ajibu kuhusu kuoa mke wa pili

Image
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, AliKiba amepata kigugumizi kuhusu kuoa mke wa pili. AliKiba kwenye mahojiano yake kwenye kipindi cha The PlayList cha Times FM amesema kuwa Mungu akijaalia we acha tu bila kutoa jibu sahihi. "Yaani unajifanya mjanja sana rafiki angu wewe, angekuwa mtu mwingine kashapitisha, sasa unatakaje Boss, utanitafutia? alihoji AliKiba. "Inshaallah Mungu akijaalia we acha tu ntakupigia shekhe wewe simu, jamani utanisaidia mimi nakwambia."

FYEKELEA MBALI ,SUKUMIA NDANI :Mimi sio mtu wa mitandao - RC Mwanri

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesema kuwa japo kuwa amekuwa ni maarufu sana kutokana na kauli zake anazozitoa katika kazi, yeye si mtu wa mitandao. RC Mwanri amesema kuwa yeye akiwa katika kazi hata yale maneno anayoyasema huwa ana tafsiri sheria na si vinginevyo. "Matukio yale unapoyaona unajua mimi sio mtu wa mitandao na Instagram na nini na Jamii Forums, ni matokeo yanayotokea kwenye field kwa kawaida ile reaction yangu ninavyosema pale inatokana na uhalisia wa jambo linalojitokeza pale kama hilo unalosema la Sukuma ndani katika Mkoa wetu wa Tabora walikuwa wanaolewa wakiwa utotoni kwahiyo pale ninapoongea pale naitafsiri sheria," Mwanri ameiambia Dizzim Online. Mkuu wa Mkoa huyo amepata umaarufu zaidi kutokana na maneno yake ya 'Sukuma ndani, Nyoosha Mkono jifanye kama unajikuna, Tutashuka nao jumla jumla, Tutapiga pasu pasu.

Picha: Rais Magufuli akiweka Jiwe la Msingi Mradi wa ujenzi wa daraja jipya

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameweka Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi Daraja Jipya na Barabara ya Aga Khan Hadi Coco Beach. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakipata maelezo toka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mhandisi Robert Mfugale kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selanderna Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Cho Tae-ick baada ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selander na Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018. Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mama Janeth Magufuli na viongozi wengine wanashuhudia Rais wa Jamhuri ...

Pata faida za kuoga maji ya moto

Image
Watu wengi hupendelea kutumia maji ya moto kuoga pale hali ya hewa inapobadilika na kuwa ya baridi au wakati mwingine mtu anaumwa hivyo anatumia maji ya moto. Sehemu kama Dar es Salaam ni mara cheche utakuta wakazi wake wanaogea maji ya moto kutokana na hali ya joto katika jiji hilo. Lakini kwa ajili ya urembo na afya ya ngozi, maji ya moto yanatajwa kuwa ni kitu muhimu sana kama vilivyo vipodozi vingine vinavyoisaida ngozi yako kuwa nyororo. Hizi hapa ni baadhi ya faida zitokanazo na matumizi ya maji  ya moto angalau mara tatu kwa wiki Kulainisha na kutunza ngozi Maji ya moto husaidia kulainisha ngozi yako tofauti na ukitumia maji ya baridi. Maji ya moto hasa yaliyo katika jakuzi ambapo utatumia muda mrefu kidogo ngozi yako ikiwa kwenye maji, husaidia kuilainisha ngozi yako na kuiweka katika hali nzuri. Usingizi Kama huwa unapata matatizo kupata usingizi usiku, amka oga kwa kutumia maji ya moto kwani husaidia kulainisha misuli ya mwili wako na itakaa sawa na utaweza...

MAGAZETI YA LEO 21/12/2018

Image

zitambue hizi dalili 5 za Tezi Dume

Image
Ugonjwa wa tezi tume imeelezwa ya kwamba ni miongoni mwa magonjwa ambayo yanasumbua jamii yetu kwa kiwango kikubwa sana na hata kupelekea kusababisha vifo. Hata hivyo tafiti mbalimbali zinazidi kuonesha ya kwamba  wanaume ambao wanatumia pombe kali kwa kiwango kikubwa wapo hatarini kupata ugonjwa huo. Licha ya wanywaji wa pombe kali lakini inasadikika ya kwamba wanaume ambao wanafanya kazi za viwandani, husasani viwanda vya rangi au wanaofanya kazi ya kupaka rangi wapo hatarini kupata  ugonjwa huo. Lakini pia wanaume ambao wapo hatarini kupata ugonjwa huo ni pamoja na wanaume wenye historia ya tatizo hili wenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zake (kaka au mdogo wa kiume) au baba kama amewahi ugua ugonjwa huu. Lakini pia watalamu mbalimbali wa masuala ya afya, wanazidi kueleza ya kwamba wanaume wenye umri wa kati ya miaka 40-70 wapo hatarini kupata ugonjwa huu wa tezi dumi. Lakini licha ya kuendelea kusambaa kwa kasi kwa ugonjwa huu w...

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL

Image
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaak Kamwelwe, amesimamisha likizo za marubani wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) katika kipindi cha mwisho wa mwaka. Amesema marubani wa ATCL ambao wameshaanza likizo wanapaswa kurudi kazini na kuendelea na kazi ya kutoa huduma kwa wananchi. Kamwelwe aliyasema hayo jana muda mfupi baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea mkoani Mbeya kwenye ukaguzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Songwe (SIA). Alisema wafanyakazi wa Mamalaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) nao hawapaswi kwenda likizo kipindi hiki cha mwisho wa mwaka bali wanapaswa kuhakikisha magari yaendayo mikoani hayapandishi nauli. "Hakuna Mtanzania atakayepata shida ya kusafiri kipindi hiki cha sikukuu. Tumejipanga kusafirisha abiria hadi usiku," alisema Waziri Kamwelwe. Alisema maofisa wa Sumatra wanapaswa kuhakikisha abiria hawaonewi wala kusumbuliwa na wenye mabasi hususani eneo l...

MAGAZETI YA LEO 20/12/2018

Image