Mahakama ya DR Congo yaidhinisha ushindi wa Felix Tshisekedi, Fayulu aitisha maandamano

Felix Tshisekedi akiwapungia mkono wafuasi wake baada ya kutangzwa mshindi wa uchgauzi
Mahakama ya katiba DR Congo imemuidhinisha rasmi Felix Tshisekedi kuwa rais wa nchi hiyo.
Mgombea aliyechukua nafasi ya pili katika matokeo ya uchaguzi wa urais nchini DR Congo Martin Fayulu ameitaka jamii ya kimataifa kutotambua matokeo hayo na ameitisha maandamano.
Taarifa yake inajiri baada ya ya mahakama ya kikatiba kuidhinisha ushindi wa mgombea mwengine wa upinzani , Felix Tshisekedi .

Muungano wa Afrika ulisema siku ya Ijumaa kwamba kulikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu matokeo hayo na kutaka matokeo rasmi kucheleweshwa.
Bwana fayulu sio mgombea pekee ambaye anaamini kwamba yeye ni muathiriwa wa wizi wa kura huku data ilioibwa ikionyesha kuwa alipata kura mara tatu ya kura alizopata Tshisekedi.
Haijulikani iwapo raia wataheshimu wito wa Fayulu wa kufanya maandamano.

Siku ya Jumatatu ujumbe wa AU unatarajiwa Kinshasa na unatarajiwa kukutana na mtu anayedaiwa 'kuiba' kura rais anayeondoka madarakani Joseph Kabila.
Iwapo Tshisekedi ataapishwa , muungano wa AU utaamua iwapo utamtambua au la.
Mahakama ya kikatiba nchini DR Congo imeidhinisha ushindi wa mgombea wa urais katika uchaguzi huo Felix Tshisekedi.
Mahakama ilikataa ombi la rufaa iliowasilishwa na Martin Fayulu ambaye ni mgombea mwengine katika uchaguzi huo wa mwezi Disemba 30.
Martin Fayulu.
Bwana Fayulu alihoji kwamba Bwana Tshisekedi alikuwa amefanya makubaliano ya kugawana mamlaka na rais Joseph Kabila, hatahivyo upande wa Tshisekedi umekana hilo.
Licha ya uamuzi wa mahakama hiyo, bwana Fayulu alisema kuwa yeye ndio mshindi wa uchaguzi huo wa urais.
Bwana Fayulu pia alihoji kwamba jamii ya kimataifa haitambui matokeo rasmi ya uchaguzi huo.
Muungano wa Afrika AU ulisema siku ya Ijumaa kulikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu matokeo ya uchaguzi huo.

Mahakama ilisemaje?

Mahakama ilisema kuwa bwana Fayulu alishindwa kuthibitisha kuwa tume ya uchaguzi ilitangaza matokeo bandia.
Iliendelea na kumtanagaza Felix Tshisekedi kuwa rais aliyechaguliwa kwa wingi wa kura. Sasa anatarajiwa kuapishwa katika kipindi cha siku 10 zijazo.
Ghasia zimetokea kila kunapokuwa na mabadiliko ya uongozi katika taifa hilo.
Lakini thibtisho la matokeo rasmi ya uchaguzi huenda likaonyesha kubadilika kwa uongozi kihalali tangu DR Congo ijipatie uhuru wake kutoka kwa taifa la Ubelgiji 1960.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja