Posts

Rais Magufuli apiga marufuku kuondoa vijiji katika hifadhi

Image
Mwandishi wetu -Dar es Salaam RAIS John Magufuli ameagiza kusitishwa hatua ya kuviondoa vijiji na vitongoji vinavyodaiwa kuwamo katika maeneo ya hifadhi. Amewataka viongozi wa wizara zinazohusika kukutana ili kuanza mchakato wa kurasimisha maeneo ya vijiji na vitongoji hivyo. Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema Rais Magufuli aliagiza viongozi wa wizara husika kubainisha maeneo ya hifadhi za wanyamapori na misitu ambayo hayana wanyamapori ama misitu ili yagawiwe kwa wafugaji na wakulima. Pia Rais ameeleza kutofurahishwa kwake na mazao kufekwa kwa kisingizo cha kupandwa ndani ya mita 60 za mito. Alitoa maagizo hayo jana alipokutana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangallah, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, (Tamisemi), Joseph Nyamhanga na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Dorothy Mwanyika. Kwa

Serikali, Airtel zaungana tena

Image
Anna Potinus – Dar es salaam Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel zimetia saini mkataba wa umiliki wa hisa na makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo ya miezi nane baina ya pande hizo mbili. Hafla ya utiaji saini imefanyika leo Januari 15, Ikulu jijini Dar es salaam na Rais Dk. John Magufuli ameshuhudia zoezi hilo ambapo Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi ametia saini kwa niaba ya Serikali na Mwenyekiti wa Kampuni ya Bart Airtel Sunil Mittal aemtia saini kwa niaba ya kampuni yake. Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini makubaliano hayo Rais Magufuli amesema kwa miaka nane Tanzania ilikua haipati gawio kutoka Bhart Airtel ilihali walikuwa na mkataba nao lakini sasa hali hiyo inaenda kubadilika kutokana na makubaliano waliyoingia. “Miaka yote nane tulikuwa hatupati gawio kutoka Bhart Airtel na ukishaona muda wote huo hatujapata ujue ni biashara mfilisi na ndio maana nilipoingia madarakani tukaliona hili tukasema tuzungumze,”

PHYSICS SYLLABUS A LEVEL

PHYSICS SYLLABUS OLEVEL I-IV

BIOLOGY FORM THREE

BIOLOGY FORM FOUR

PHYSICS FORM ONE

PHYSICS FORM THREE

PHYSICS FORM TWO

Mbunge kuwasilisha hoja binafsi lugha ya kufundishia

Image
TIGANYA VINCENT, TABORA MBUNGE wa Tabora Kaskazini,  Almas Maige (CCM), amesema wakati umefika kwa Watanzania kuanza kutumia   Kiswahili kwa ajili ya kufundishia katika shule za sekondari na elimu ya juu kwa masomo yote. Amesema hatua hiyo itasaidia kuwawezesha vijana wengine kuelewa wanachofundishwa na kuwa na ufanisi katika utendaji kazi. Maige alisema hayo jana mjini Tabora alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu hoja yake aliyoiwasilisha bungeni  kutaka Kiswahili kitumike kama lugha ya kifundishia na kujifunza katika shule za sekondari na vyuo  nchini. Alisema utafiti uliofanywa na wataalamu na wanazuoni mbalimbali umeonyesha  asilimia 50 ya wanafunzi hawaelewi wanachofundishwa kutokana na matumizi ya Kiingereza. Maige alisema hata wanavyuo vya ufundi wanaofundishwa kwa   Kiingereza wanapomaliza masomo yao wanapokuwa kazini hawatumii lugha hiyo katika kutekeleza  majukumu yao ya kila siku bali wanatumia Kiswahili. Mbunge huyo wa Tabora Kaskazini a

PHYSICS FOR FOUR

BIOLOGY FORM ONE

CHEMISTRY FORM ONE

ACADEMIC BOOKS

Image
               <<<  OPEN HERE  BIOLOGY FORM TWO BIOLOGY FORM THREE   BIOLOGY FORM FOUR     <<OPEN HERE>>   <OPEN HERE>>                                        <<PHYSICS FORM FOUR>> <<PHYSICS FORM THREE>> <<PHYSICS FORM TWO >> <<PHYSICS FORM ONE>> PHYSICS SYLLABUS O- LEVEL     PHYSICS SYLLABUS A-LEVEL  BIOLOGY SYLLABUS O-LEVEL    BIOLOGY SYLLABUS A- LEVEL CHEMISTRY SYLLABUS O-LEVEL CHEMISTRY SYLLABUS A-LEVEL GEOGRAPHY SYLLABUS O-LEVEL GEOGRAPHY SYLLABUS A-LEVEL

CHEMISTRY FORM THREE

HABARI ZA LEO JUMAPILI 13/1/2019

Image

Waziri awaonya madaktari nchini

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewaonya madaktari kote nchini kuacha tabia za kuwa madalali wa Maduka ya dawa kwa kuwaandikia wagonjwa dawa mara mbili mbili. Waziri Ummy ameagiza hospitali za Rufaa kote nchini kuhakikisha zinakuwa na maduka ya dawa litakalokuwa  na uhakika wa dawa zote muhimu ili kuondosha kero hiyo na kuondoa mianya ya madaktari kudalalia dawa kwenye maduka binafsi. Hata hivyo amesema kuwa watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Waumini wamgeuka Imam msikitini, wataka aongoze maandamano

Image
Imam mwenye ushawishi mkubwa jijini Khartoum nchini Sudan amezongwa na waumini akiwa msikitini wakimtaka awaongoze kufanya maandamano dhidi ya Serikali ya Rais Omar al-Bashir. Video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii inawaonesha baadhi ya waumini wakipaza sauti mbele ya Imam huyo, “amka utuongoze kuandamana kutoka hapa msikitini.” Umati wa watu walitoka msikitini wakipiga kelele za kutaka Serikali iliyopo madarakani iachie ngazi. Polisi waliofika katika eneo hilo walifyatua mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji waliojikusanya baada ya ibada ya Ijumaa. Katika kipindi cha wiki mbili za maandamano ya kupinga Serikali, watu 22 wameripotiwa kupoteza maisha. Okwi, Kagere walivyowapasua JS Saoura 3-0 Kwa mujibu wa Reuters, maandamano yaliyoshuhudiwa jana ni makubwa kuliko yaliyokuwa yamefanyika awali. DC Njombe awapa neno Wajasiliamali Maandamano yalianza Desemba 19 mwaka huu baada ya Serikali kutangaza kupanda kwa bei za vyakula na mafuta, hali inayoda

Mpinzani apinga matokeo ya Urais wa DRC Mahakamani

Image
Aliyekuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa tiketi ya chama cha upinzani, Martin Fayulu amefungua kesi katika Mahakama ya Kikatiba akipinga matokeo ya uchaguzi wa nchi hiyo. Tume ya Huru ya Uchaguzi ya Taifa (CENI), ilimtangaza mgombea mwingine wa upinzani Felix Tshisekedi kuwa mshindi wa uchaguzi huo uliofanyika Desemba 30 mwaka jana. Kwa mujibu wa takwimu za CENI, Tshisekedi alipata kura milioni 7 huku Fayulu akipata kura milioni 6.4 na mgombea wa chama tawala mmanuel Shadary akiambulia kura Milioni 4.4. Feli Ekombe ambaye ni mwanasheria wa Fayulu amesema kuwa katika kesi hiyo, mteja wake anataka Mahakama ifute matokeo yaliyotangazwa na CENI yanayombua Tshisekedi kama Rais mteule wa taifa hilo la Afrika ya Kati. Marekani, Ufaransa na Uingereza vimetaka kutoa ufafanuzi wa kina wa namna matokeo hayo yalivyopatikana. Wiki iliyopita, Kanisa Katoliki lenye ushawishi mkubwa nchini humo, kupitia kwa Baraza la Maaskofu lilieleza kuwa matokeo yaliyotanga

Makumi wapoteza maisha kwenye mlipuko wa tenki la mafuta

Image
on Makumi wapoteza maisha kwenye mlipuko wa tenki la mafuta Watu kumi na wawili wamepoteza maisha nchini Nigeria baada ya tenki la mafuta kulipuka mwishoni mwa wiki, kwa mujibu wa taarifa ya polisi. Tukio hilo limesababisha vifo vya watu kutokana na mlipuko wa matenki ya mafuta nchini humo kufikia mamia ndani ya kipindi cha miaka ya hivi karibuni, kutokana na watu kutoboa matenki hayo kwa lengo la kukusanya mafuta. “Tumekusanya miili 12 ya watu waliopoteza maisha pamoja na watu 22 waliojeruhiwa vibaya kutokana na kuungua na tumewapeleka hospitalini,” msemaji wa Polisi, Irene Ugbo ameiambia Associated Press jana. Amesema kuwa mlipuko huo ulitokea Ijumaa jioni katika eneo la Odukpani kwenye jimbo la Cross River. Baadhi ya mashuhuda waliohojiwa wamedai kuwa idadi kuwa idadi ya waliopoteza maisha wanafikia 60 na kwamba miili mingine haikuchukuliwa na polisi.