Makumi wapoteza maisha kwenye mlipuko wa tenki la mafuta Skip to main content

Makumi wapoteza maisha kwenye mlipuko wa tenki la mafuta


on Makumi wapoteza maisha kwenye mlipuko wa tenki la mafuta
Watu kumi na wawili wamepoteza maisha nchini Nigeria baada ya tenki la mafuta kulipuka mwishoni mwa wiki, kwa mujibu wa taarifa ya polisi.
Tukio hilo limesababisha vifo vya watu kutokana na mlipuko wa matenki ya mafuta nchini humo kufikia mamia ndani ya kipindi cha miaka ya hivi karibuni, kutokana na watu kutoboa matenki hayo kwa lengo la kukusanya mafuta.
“Tumekusanya miili 12 ya watu waliopoteza maisha pamoja na watu 22 waliojeruhiwa vibaya kutokana na kuungua na tumewapeleka hospitalini,” msemaji wa Polisi, Irene Ugbo ameiambia Associated Press jana.
Amesema kuwa mlipuko huo ulitokea Ijumaa jioni katika eneo la Odukpani kwenye jimbo la Cross River.
Baadhi ya mashuhuda waliohojiwa wamedai kuwa idadi kuwa idadi ya waliopoteza maisha wanafikia 60 na kwamba miili mingine haikuchukuliwa na polisi.

Comments

Popular posts from this blog

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL