Wanafunzi 133, 000 waliofaulu, wakosa madarasa sekondari
WANAFUNZI 133,747 sawa na asilimia 18.24 waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu hawakupata nafasi ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari za serikali kwamwaka 2019 kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa. Akizungumza jana Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Seriklali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo alisema wizara hiyo imekamilisha zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wanaopaswa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani ambapo jumla ya wanafunzi 599,356 sawana asilimia 81.76 wamechaguliwa kati ya733,103 waliofaulu. “Aidha jumla ya wanafunzi 133,747 sawa na asilimia na asilimia 18.24 ya waliofaulu hawakupata nafasi kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa,”alisema Jafo. Jafo alitaja mikoa 17 ambayo ina uhaba wa vyumba vya madarasa na idadi ya wanafunzi waliobaki ni pamoja na Arusha wamebaki wanafunzi 18, 719, Dodoma wanafunzi 5, 991, Iringa wanafunzi 2,774 , Kagera wanafunzi 14, 046, K...