Mikopo mingi chechefu inatokana na wafanyakazi wa benki wasio waaminifu’





                Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga, amebainisha sababu za benki kutokopesha linatokana na benki zenyewe kutokuwa na wafanyakazi waaminifu kwa kuruhusu wakopaji wasiokidhi vigezo na kusababisha mikopo chechefu.
Kutokana na hali hiyo, amesema BoT imechukua jukumu la kufuatilia kuajiriwa kwa watumishi hao pamoja na mambo mengine.
                              Profesa Luoga amesema hayo leo Jumatatu Desemba 10, katika mkutano wa Rais John Magufuli na uongozi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).
“Ni kweli benki zinapaswa kuwa huru lakini BoT inapaswa kuangalia mwenendo wao, kwa mfano kuna wakati mikopo ilikuwa haitolewi, BoT imechukua jukumu na imekuwa ikikaa chini na benki nchini kutathmini kwanini mikopo haitolewi na mara nyingi majibu na kwamba benki inaogopa hasara kwa sababu watu hawajulikani lakini BoT imechukua jukumu kuhakikisha watu wanajulikana.
“Pia kumekuwa na tatizo la rushwa, wakopaji wengine wabovu wamekuwa wakihonga ili wakopeshwe sasa tunajiuliza inakuwaje benki inamkopesha mkopaji mbovu,” amesema.
Pamoja na mambo mengine, Profesa Luoga amesema kumekuwa na tatizo la wafanyakazi wasio na uwezo au ujuzi usiotakiwa kwani si rahisi kuwa benki inakopesha kwa mradi ambao mkopo wake haurudishiki.
“Pale inapoonekana benki haina watu wenye weledi katika uongozi BoT itaendelea kutoa masharti kuwa watu wote lazima wawe na watumishi stahiki,” amesema.

Comments

Popular posts from this blog

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL