Magufuli atoa vitambulisho maalumu kwa wafanyabiashara wadogo
Rais John Magufuli, amezindua vitambulisho maalumu 670,000 kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo ili viwasaidie kuzitambulisha biashara zao.
Rais Magufuli amegawa vitambulisho hivyo leo Jumatatu Desemba 10, alipokuwa katika mkutano wake na viongozi wa Mamlaka yaMapato (TRA) na wakuu wa mikoa ambapo amesema vitambulisho hivyo ni maalumu kwa wafanyabiashara ambao mtaji wao hauzidi Sh milioni nne.
Baada ya kugawa vitambulisho hivyo maalumu kwa wakuu wa mikoa ili wakawapatie wafanyabiashara katika maeneo yao, Rais Magufuli ametaka wafanyabiashara hao wasisumbuliwe na mtu yeyote.
“Nimefikia hatua ya kutoa vitambulisho hivyo mimi mwenyewe kwa sababu nimeona mamlaka husika inachelewesha na wafanyabiashara wadogo wanaendelea kusumbuliwa.
Rais Magufuli amesema vitambulisho hivyo viko 670,000 na kila mkuu wa mkoa atapewa vitambulisho 25, 000 ili wakavigawe kwa wafanyabiashara wa maeneo yao na fedha watakazopewa wakazilipe TRA.
“Vitambulisho hivi navitoa bure ila wafanyabishara watachangia 20,000 kila mmoja, kama kurudisha gharama yautengenezwaji wake ili fedha hizo zikatumike kutengenezea vitambulisho vinginena kianze kutumika mara tu anapokipata.
“Kama vitambulisho hivi navitoa mimi mwenyewe sijaona mtu wa kuwasumbua, na mfanyabiashara mwenye mtaji wa chini ya Sh 4,000, 000 naana kitambulisho nasisitiza asisumbuliwe,” amesema.
Aidha Rais Magufuli ametoa rai kwa wafanyabiashara watakaopata vitambulisho hivyo kuvitumia kwa matumizi yao si kuvichukua kisha wakawafanyie biashara wafanyabiashara wakubwa.
Comments