Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC
Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC Na Upendo Mosha-Moshi MKUU wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Kippi Warioba, ametuhumiwa na wananchiwa Kijiji cha Chekereni Weruweru, Kata ya Kindi kuvamia na kuvunja ofisi ya kijijihicho na kuchukua nyaraka mbalimbali. Kutokanana hali hiyo wananchi hao wametishia kumfikisha mahakamani kwa madai ya kuvunja kufuli la ofisi ya kijiji na kuchukua nyaraka hizo. Mwenyekiti wa kijiji hicho, John Bosco, aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana kijijini hapo. Bosco alisema kiongozi huyo amekuwa ni sehemu ya kuchochea migogoro na kwamba hawapotayari kuchonganishwa bali watafuata sheria. Alisema mgogoro huo ulianza baada ya mkuu huyo wa wilaya, kutumia nguvu nakuwanyang’anya kijiji ofisi yake na kukipa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jambo ambalo ndio chanzo cha mgogoro huo. “Tunataka mahakama itafsiri kuwa ofisi ya Kijiji cha Chekereni Weruweru ni mali ya Serikaliya kijiji au CCM… mk...
Comments