Posts

Showing posts from December, 2018

VIDEO: Mrisho Gambo kutua na tuzo kwa Rais Magufuli

Image
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amekabidhiwa Tuzo maalum kwa ajili kwenda Rais Magufuli ambapo ni shukrani zao kwa ajili ya kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi cha miaka mtatu tangu aingie madarakani.  PATA MAARIFA ZAIDI

Fahamu faida za Kitunguu Maji mwilini mwako

Image
Kitunguu maji ni aina ya mboga yenye harufu kali inayochangamsha mwili. Pia kitunguu ni kiungo ambacho kina virutubisho katika vyakula na kuvifanya viwe na ladha nzuri. Nchi mashuhuri na maarufu inayolima kiungo hicho ni Misri na kusambaa zaidi duniani na nchini Tanzania kinalimwa zaidi katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Arusha na mikoa mingine ambayo ina rutba nzuri ya kustawisha kiungo hicho. Kiungo hicho kimekuwa kikitibu na kuponya maradhi mbalimbali kutokana na kuwa na salfa ambayo ni nzuri, hasa kwenye ini na husaidia kuponya kansa kwenye utumbo na kinywa kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya vitamini C. Kitunguu maji kina kazi nyingi katika mwili wa binaadamu, kwani hutibu magonjwa mbalimbali, ikiwemo kikohozi, vidonda vya tumbo na mifupa, ngozi koo, figo, tumbo na mkojo, kufunga hamu ya kula, hutia kiu na hulainisha tumboni. Pia, kitunguu maji ni chanzo cha madini mengi ambayo yanapatikana katika kiungo hicho ambayo yana umuhimu mkubwa ...

HABARI KUBWA MAGAZETINI LEO30/12/2018

Image
   PATA MAARIFA ZAIDI

PIGO JINGINE:Dkt. Mashinji na wenzake watatu waswekwa ndani

Image
Dkt. Mashinji na wenzake watatu waswekwa ndani Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji na viongozi wengine watatu wa chama hicho wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Hai, Mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali. Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Hai ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya ambapo amesema kuwa viongozi hao wamekamatwa mchana kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usiokuwa halali. “Ni kweli tumemkamata Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Mashinji, katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Basir Lema, mwenyekiti wa halmashauri ya Hai, Egra Mchomvu na msaidizi wa mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, Irine Lema kwa kufanya mkusanyiko usio halali,” amesema. Amesema kuwa viongozi hao, wamekutwa wakifanya mkusanyiko katika eneo la Boma bila ya kuwa na kibali jambo ambalo ni kinyume cha sheria. ...

HapoKale: Wachaga na kisa cha kurudi nyumbani kila mwisho wa mwaka

Image
  Wachaga na kisa cha kurudi nyumbani kila mwisho wa mwaka Wachaga ni kabila lenye asili ya Kibantu na mchanganyiko wa asili ya Kikushi wanaoishi kaskazini mwa Tanzania, Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro. Kabila la Wachaga linatajwa kuwa la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania, ambapo takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachaga ni watu 2,000,000. Shughuli kubwa ya Wachaga ni biashara, kilimo na kazi za ofisini. “Mangi” ni jina waliloitwa watawala wa Kichaga. Hawa walimiliki mashamba, Ng’ombe na waliheshimiwa kama viongozi wa kikabila. Mangi walikuwa na nguvu za kisiasa na utajiri. Baadhi ya Mangi mashuhuri katika historia ni Mangi Rindi aliyeingia mikataba na wakoloni (Wajerumani), Mangi Sina wa Kibosho – anajulikana kwa uhodari wake wa vita katika kupigana na Wamachame na kupora ng’ombe na mazao yao, ...

Liverpool yaipasua Arsenal, Firmino achoma kibanda cha bunduki

Image
Liverpool yaipasua Arsenal, Firmino achoma kibanda cha bunduki Klabu ya Liverpool jana imeipasua Arsenal kwa kipigo cha 5-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza, ushindi ulioiwezesha kujikita zaidi kileleni huku ikitishia usalama wa wapinzani wake. Arsenal ilikuwa ya kwanza kuchokoza nyavu za Liverpool katika dakika ya 11 baada ya Ainsley Maitland-Niles kupata upenyo na kujikita ndani ya 18 akiwaacha walinzi wa Liverpool kwa mbali. Lakini jua lililoonekana mbele ya Unai Emery halikuwa la machweo bali lilikuwa la alfajiri na kazi ilikuwa inaanza. Liverpool walijibu dakika tatu baadaye kupitia kwa Roberto Fermito aliyetumia makosa ya safu ya ulinzi ya washika bunduki hao iliyojichanganya. Hata hivyo, Fermito hakuwaacha wanywe maji kwa mshangao wa msawazisho na alipachika goli la pili katika dakika ya 16 ikiwa ni dakika mbili tu tangu ashangilie goli la kwanza. Mvua ya magoli ilianza kufunguka taratibu dhidi ya Arsenal, a...

TANZIA: Mwanasiasa mkongwe nchini afariki dunia

Image
16 hours ago Comments Off on TANZIA: Mwanasiasa mkongwe nchini afariki dunia Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Pancras Ndejembi amefariki dunia leo Jumamosi Desemba 29, 2018 majira ya saa 3:30 asubuhi. Ndejembi amefariki katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alikopelekwa kwaajili ya matibabu baada ya hali yake kubadilika ghafla. Aidha, mtoto wa Marehemu, Edna Ndejembi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, huku akisema baba yake alikuwa anasumbuliwa na kifua kubana ambapo alilazwa katika Hospitali ya DCMC ya jijini Dodoma na kuruhusiwa juzi Alhamisi akiwa ameimarika kiafya. “Lakini jana jioni hali yake ilibadilika ghafla ndipo tukamkimbiza hapo hospitali ya mkoa na leo saa tatu asubuhi mzee ametutoka,” amesema Edna. Hata hivyo, Mzee Ndejembi aliwahi kuwa mkuu wa wilaya mbalimbali nchini na baadaye akawa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa ...

MAKTABA -PAST PAPERS

MAKTABA -PAST PAPERS FORM SIX MAKTABA PAST PAPERS FORM FOUR  MAKTABA -PAST PAPERS FORM TWO MAKTABA PRIMARY

PHYSICS 2B F4-2010

PHYSICS 2B F4 -2011

PHYSICS 2B F4-2012

PHYSICS 2B F4-2013

PHYSICS 2C F4-2010

PHYSICS 2B F4-2017

PHYSICS 2B F4-2016

PHYSICS 2B F4-2015

PHYSICS 2C F4-2011

PHYSICS 2C F4-2012

PHYSICS 2C F4-2013

PHYSICS 2C F4 2014

PHYSICS 2C F4-2015

CLASSIFICATION OF LIVING THINGS -FORM FOUR

HIV -AIDS-STIs FORM FOUR

GROWTH FORM FOUR

GENETICS FORM FOUR

BIOLOGY FORM TWO -NOTES

BIOLOGY FORM ONE NOTES

QUAGS -O-LEVEL

BIOLOGY PRACTICAL NOTES

QUAGS-ACSEE

PRINCIPLE OF PHYSICS S.CHANDS CLASS XII

Askari aua mke kwa kumpiga risasi

Image
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma, linamshikilia askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wa kikosi cha Chandarua Sajenti Batisin Samda, kwa tuhuma za kuwauwa kwa kuwapiga risasi watu wawili akiwamo mtalaka wake. Askari huyo alitekeleza mauaji hayo akiwa kazini kwa kumuua askari mwenzake, Sajenti Juma Mkele na mtalaka wake, Veronica Kayombo. Akizungumza na Nipashe jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Gemini Mushy, alisema tukio lilitokea juzi majira ya saa 10 alasiri kwenye eneo la kambi hiyo. Kwa mujibu wa Kamanda Mushy, inadaiwa kuwa Kayombo alikuwa amekwenda kwenye kambi hiyo kumpelekea hati ya wito kutoka idara ya ustawi wa jamii aliyekuwa mume wake, jambo ambalo linaonyesha lilisababisha askari huyo kupandwa na hasira. Alisema siku hiyo ya tukio, Kayombo alipofika kwenye kambi hiyo, kabla ya kukutana na Samda, alionana na mkuu wake wa kazi na baadaye mkuu huyo alimpa maagizo Sajenti Mkele ili ampeleke kwake (Samda) akamkabidhi barua hiyo ya wito. Kaman...

MBINU ZA KUFAULU MTIHANI KWA WANAFUNZI

Image
Ili mwanafunzi aweze kufaulu mtihani lazima afanye yafuatayo 1.Mtihani ni nini? 2.kwanini kuna mtihani? 3.anayetunga mtihani ninani? 4.mtihani unajibiwa na nani? 5.mbinu gani za kujibu mtihani? 6.Mtihani unajibiwa ukiwa na hali gani (mud) 7.Nitafanyeje ili niweze kufaulu mitihani yangu? 8.Nifanyeje kabla ya kuingia kwenye chumba cha mtihani? 9.Nikina nani wanapaswa kufaulu mtihani? Akijua maswali haya mwanafunzi atajijengea juhudi ya kusoma ili afaulu zaidi KUMSAIDIA MWANAFUNZI AFAULU SAYANSI   BONYEZA HAPA

VIDEO: JPM AFYEKLEA MBALI FORMULA MYA SAKATA LA KIKOKOTOO

Image
Rais Magufuli ameamuru mifuko ya hifadhi ya jamii iendelee na kikokotoo kilichokuwa kikitumika kwa kila mfuko kabla ya mifuko hiyo kuunganishwa kiendelee hadi mwaka 2023 ambapo inakadiriwa kuwa wanachama takriban 58,000 ndiyo watakaostaafu katika kipindi hicho. SAIDIA WENGINE

BREAKING NEWS: Rais Magufuli 'amtumbua' Mkurugenzi wa SSRA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa SSRA, Dkt. Irene Isaka.   BONYEZA HAPA UWASAIDIE WENGINE

RC Makonda atoa zawadi ya thamani ya sh. milioni 72

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo ametoa zawadi ya kufunga mwaka ya Ng'ombe 60 wenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 72 kwa Jeshi la Wananchi JWTZ,  Jeshi la Polisi, Hospital ya Taifa Muhimbili, Ocean Road na Hospital za Mkoani humo kama chachu ya kuongeza morali ya kazi katika kuwahudumia wananchi. Katika mgawanyo huo Jeshi la wananchi JWTZ wamepata Ng'ombe 20,Jeshi la Polis Ng'ombe 20 na Sekta ya Afya Ng'ombe 20 ambapo RC Makonda amesema anafurahishwa sana na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na vyombo hivyo. RC Makonda amesema Ng'ombe aliowakabidhi sekta ya Afya wataenda kula Madaktari, Wauguzi na wagonjwa watakaokuwa wodini kwenye hospital zote za Mkoa huo ikiwemo Muhimbili, Ocean road, Amana, Mwananyamala na Temeke ambapo RC Makonda ametoa nyama hiyo Kama zawadi ya sikukuu na pole kwa wagonjwa. Aidha RC Makonda amevipongeza vyombo vya ulinzi na Usalama kwa kusimamia hali ya usalama jijini humo kuwa shwari masaa 24 na kuwafan...

Pata faida :Kwanini utumie nanasi kwa wingi?

Image
Kwa mara nyingine tena Muungwana blog inakuja tena mbele ya macho yako ili uweze kusoma makala haya, ambapo siku ya leo tutazungumza ni kwanini ni muhimu kula nanasi kwa wingi. Kwanza kabisa unatakiwa kuelewa ya kwamba tunda la nanasi lina wingi wa vitamin A, B, C pia lina mkusanyiko wa madini ya Chuma, calcium, copper na phosphorous pia watalamu mbalimbali wa maswala ya afya wanatusahauri tule tunda hili kwani linasaidia sana kuimarisha mifupa na misuli ya mwili. Zifuatazo ndizo sababu ya kwanini uendelee kula tunda la nanasi: Husaidia kwa kiwango kikubwa kuongeza wingi wa maziwa kwa akina mama wanyonyeshao, hivyo ni muhimu kwa watu hawa kuendelea kula matunda haya ili kuongeza kiwango kingi cha maziwa. Kwa wale wenye matatizo ya upungufu wa damu mwili basi tunda hili husaidia sana katika suala kuongeza damu mwili. Pia kama unamatatizo ya kufunga kwa choo basi unashauriwa kuendelea kutumia tunda hili  la nanasi kwani linauwezo mkubwa  wa kuwez...

MAGAZETI YA LEO 29/12/2018

Image