Pata faida :Kwanini utumie nanasi kwa wingi?




Kwa mara nyingine tena Muungwana blog inakuja tena mbele ya macho yako ili uweze kusoma makala haya, ambapo siku ya leo tutazungumza ni kwanini ni muhimu kula nanasi kwa wingi.

Kwanza kabisa unatakiwa kuelewa ya kwamba tunda la nanasi lina wingi wa vitamin A, B, C pia lina mkusanyiko wa madini ya Chuma, calcium, copper na phosphorous pia watalamu mbalimbali wa maswala ya afya wanatusahauri tule tunda hili kwani linasaidia sana kuimarisha mifupa na misuli ya mwili.

Zifuatazo ndizo sababu ya kwanini uendelee kula tunda la nanasi:
Husaidia kwa kiwango kikubwa kuongeza wingi wa maziwa kwa akina mama wanyonyeshao, hivyo ni muhimu kwa watu hawa kuendelea kula matunda haya ili kuongeza kiwango kingi cha maziwa.

Kwa wale wenye matatizo ya upungufu wa damu mwili basi tunda hili husaidia sana katika suala kuongeza damu mwili.

Pia kama unamatatizo ya kufunga kwa choo basi unashauriwa kuendelea kutumia tunda hili  la nanasi kwani linauwezo mkubwa  wa kuweza kutibu tatizo hilo kwa asilimia mia moja.

Kula nansi kwa wingi kwa sababu nanasi huasaidia kwa kiwango kikubwa kuweza kutibu matatizo yote kusahausahau, kula nanasi kwa wingi kwa sababu nanasi husaidia kuongeza uwezo wa kukumbuka mambo mbalimbali.

Ulaji wa nanasi hutibu matatizo yote ya tumbo  pamoja na mataizo ya bandama, hivyo kula matunda kwa wingi ili kujibu.

Mwisho Muungwana blog inakusisitizia ya kwamba unatakiwa kula nanasi kwa wingi kwani ni muhimu sana katika afya zetu. Usiburi daktari akwambie uanze kula matunda bali unachotakiwa kufanya nia kuanza kula matunda hayo kuaznia sasa.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja