Posts

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KUSOMA "DEGREE" BILA KUPITA "FORM SIX".

Image
Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Pro.Joyce Ndalichako amepiga marufuku wanafunzi kujiunga na masomo ya Shahada (degree) bila kupita kidato cha sita. Marufuku hiyo itaanza rasmi katika mwaka ujao wa masomo. Prof.Ndalichako emesema mfumo wa elimu huria umechangia kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma. Ndalichako amesema wanafunzi wanaofeli kidato cha nne na kwenda kusoma certificate na baadae diploma ili wajiunge vyuo vikuu hawataruhusiwa kujiunga na masomo ya shahada (degree) kama hawajarudia (reseat) masomo yao na kupata alama za kwenda kidato cha tano, na wafanye mitihani ya kidato cha sita na kufaulu ndipo wajiunge vyuo vikuu. Katika utaratibu huo, wanafunzi wa kidato cha nne watakaoruhusiwa kusoma shahada (degree) bila kupita kidato cha 5 na 6 ni wale waliofaulu kidato cha 4 na wakachaguliwa kwenda kusoma katika vyuo vya ufundi daraja la kati (Technicians). Lakini wale wanaokosa "credit" za kuendelea form five na kuamua kwenda certificate mw...

NEW ANOUNCEMENT:PRACTICALS ,PRACTICALS ,PRACTICALS

WADAU WOTE WA ELIMU MNATANGAZIWA KUWA ,NOTES ZA MASOMO YA SAYANSI KWA VITENDO (PRRACTICAL) BIOLOGY ,PHYSICS, CHEMISTRY KWA UPANDE WA OLEVEL, ZINAPATIKANA HAPA ZINGINE PIA

NEW: TIME TABLE JANUARY -2019 NOW IS OUT

Udhaifu' wa Bunge wamponza CAG na Mdee

Image
Spika wa Bunge Job Ndugai (Mb) amemtaka  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad  na  Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee kufika  mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kujieleza kufuatia kauli za kudhalilisha Bunge. Kushoto ni CAG Prof. Mussa Assad, kulia ni Mbunge wa Kawe Halima Mdee Taarifa iliyotolewa na Mhimilili huo imesema kwamba viongozi hao wamelidhalilisa bunge kwa kuliita kuwa ni dhaifu ambapo Prof. Assad alitoa kauli hiyo akiwa nje ya nchi. Spika Ndugai ametaka Mussa Assad, CAG afike mwenyewe kwa hiyari yake mbele ya kamati ya maadili ya Bunge tarehe 21. 01.2019 vingenevyo atapelekwa kwa pingu huku Mdee akitakiwa kwenda tarehe 22. Hivi Karibuni CAG akijibu swali la  Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alisema kitendo cha ofisi yake kufanya ukaguzi na kutoa ripoti zenye kuonyesha kuna ubadhirifu lakini baada ya hapo wananchi hawa...

Zitto awaponza viongozi wa ACT Wazalendo

Image
Jeshi la Polisi Wilayani Kigoma linawashikilia viongozi watatu wa Ngome ya Vijana Jimbo la Kigoma Mjini waliokwenda polisi kutoa taarifa ya kufanya maandamano ya amani. Zitto Kabwe Ngome hiyo ya vijana imeeleza kuwa mpaka sasa hakuna taarifa rasmi ya sababu gani polisi imewashikilia viongozi hao wa Vijana Kigoma Mjini huku ikidai kuwa huenda wakakosa kabisa dhamana kwa siku ya leo. Viongozi wanaoshikiliwa na Polisi ni Said Mlindwa (Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Jimbo), Wakili Mubanga (Katibu wa Ngome ya Vijana Jimbo) na Ntakije Ntanena (Katibu Mwenezi wa Ngome ya Vijana Jimbo) Maandamano ambayo walikuwa wameenda kuyaombea kibali ni ya amani kwaajili ya  kumpongeza Mbunge wao Zitto Kabwe na madiwani kwa kazi wanayoifanya kuwaletea wananchi maendeleo. Aidha Ngome hiyo ya Vijana imesisitiza kuwa inawaombea dhamana kwakuwa ni haki yao na wanapaswa kupewa kwa kuwa masharti ya dhamana kwa mujibu wa sheria yametimizwa.

Wastaafu waandamana hadi NSSF kushinikiza walipwe mafao yao

Image
Bethsheba Wambura, Dar es Salaam Zaidi ya wanachama 200 wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), wamekusanyika katika Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni wakishinikiza kulipwa mafao yao. Wastaafu hao wamekusanyika leo kuanzia saa sita mchana katika ofisi hizo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, ambapo wako waliostaafu kuanzia mwaka jana kurudi nyuma ambapo pamoja na mambo mengune wamedai hawajui ni kwanini hawalipwi mafao yao wakati Rais John Magufuli ametangaza wapewe mafao yao kwa wakati. Akizungumza na Mtanzania Digital mmoja wa wastaafu hao, Khamis Khamis, amesema yeye amestaafu tangu Juni mwaka 2018 lakini kila anapoenda kudai mafao yake anapigwa tarehe hali inayomfanya anashindwa kulipia watoto ada za shule ama kufungua biashara. Amesema wamekusanyika ili kupatiwa stahiki zao huku wakishinikiza kitumike kikotoo cha zamani na sio kile cha asilimia 33.3 kwani mtu anakuwa anadai fedha nyingi ila anapewa kidogo sababu tu sheria hairuhusu wakati Rais Magufuli alisema kila anayestaaf...

MAGAZETI YA LEO 8/1/2019

Image
Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 8, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 7, 2019

Image
Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 7, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

MGOMO: Mrema awagumzo kwa wapinzani wenzake

Image
AZIZA MASOUD – Dar es Salaam MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema, amesema hawezi kuungana na vyama vingine vya upinzani vilivyofungua kesi kupinga Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018. Amesema anaamini kufanya hivyo hakuwezi kuondoa matatizo yaliyopo ambayo msingi wake unatokana na ubovu wa sheria zilizopo. Mrema ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja kupita baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuanza kusikiliza kesi namba 31 ya kupinga muswada huo iliyofunguliwa mahakamani hapo Desemba 20 mwaka jana na viongozi wa vyama vya upinzani. Viongozi hao ni Kiongozi Mkuu ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, Kaimu Katibu Mkuu Cuf (Bara), Joram Bashange na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa chama hicho, Salim Bimani. Katika kesi hiyo mshtakiwa mkuu ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Adelardus Kilangi. Akizungumza na waandishi wa habari jana nyumbani kwake Salasala, Dar es Salaam, Mrema alisema wapinzani wanapaswa kufahamu kuwa hitaji la sasa...

Makamu Mwenyekiti wa chama tawala Kenya ajiuzulu

Image
Makamu Mwenyekiti wa chama tawala cha Jubilee nchini Kenya, David Murathe amejiuzulu wadhifa wake huo. Lakini akanusha taarifa zilizojitokeza kwamba amejiondoa kwenye chama hicho.

Mlipuko wa bomu wauwa polisi mmoja

Image
Polisi mmoja ameuawa katika mlipuko karibu na kanisa mashariki mwa Cairo nchini Misri. Bomu lililotegwa kwa mikono karibu na Kanisa la Abu Seyfeyn huko Cairo lililipuka ghafla wakati polisi wakijaribu kulitegua na kusababisha kifo cha polisi mmoja. Polisi watatu wameripotiwa kujeruhiwa.

Tumbua tumbua: vigogo Ardhi Kigoma wavuliwa nyadhifa

Image
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Dk. Angelina Mabula amewavua nyadhifa wakuu wa Idara ya Ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi ipasavyo. Waliovuliwa nyadhifa hizo ni Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Manispaa ya Kigoma, Brown Nziku, Mkuu wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Emanuel Magembe na Ofisa Ardhi Mteule, Paul Misuzi. Mabula alifanya uamuzi huo Januari 3, mwaka huu akiwa mkoani hapa baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma. Alifikia uamuzi huo baada ya watendaji hao kushindwa kusimamia maagizo na maelekezo yaliyotolewa tangu mwaka juzi kuhusu ukusanyaji wa kodi ya ardhi, uingizaji wa wamiliki wa viwanja na mashamba kwenye mfumo wa malipo kwa njia ya kielekroniki wa ardhi na utoaji wa hati za madai kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi. Mabula alisema pamoja na barua iliyoandikwa na Kamishna wa Ardhi Msaidiz...

TAHARUKI: KANISA KATOLIKI LAANIKA HADHARANI JINA LA MSHINDI WA URAIS CONGO

Image
Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (Cenco), lenye ushawishi mkubwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limesema linafahamu aliyeshinda uchaguzi wa rais ambao ulifanyika Desemba 30 mwaka jana na kuomba Tume ya Uchaguzi (CENI) kutangaza matokeo katika mazingira huru, haki na ukweli. Baraza hilo limetoa baada ya tume ya uchaguzi kutangaza kwamba italazimika kuchelewa kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita kutokana na hitilafu za kimitambo. Kanisa hilo limesema sampuli ya wawakilishi ilichapishwa katika vituo vya kupigia kura ambavyo vinawaruhusu kujua jina la rais aliyechaguliwa. Sampuli hiyo ni ya vituo zaidi ya 23,000 kati ya vituo 70,000 vilivyowekwa na Ceni nchini humo. Akizungumza na vyombo vya habari nchini humo, msemaji wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki, Padri Donatien Nshole, amesema si jukumu lao kutangaza matokeo, bali wao ni waangalizi lakini wanafahamu nani aliyechaguliwa na wananchi. “Ni muhimu kusisitiza kuwa k...

WATANO WAGONGWA NA LORI WAKITOKA HARUSINI, WAFARIKI – VIDEO

Image
AJALI mbaya ya lori la mchanga lenya namba za usajili T155 ATC kugongana na gari la abiria aina ya Toyota Hiace imetokea majira ya saa 8 usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Januari 5, 2019 katika maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambapo lori hilo limeacha njia na kutumbukia mtaroni. Kutokana na taarifa ambazo hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi, inadaiwa kuwa lori hilo liliigonga Hiace ikiwa imebeba watu wengi waliyokuwa wakitoka kwenye harusi na kusababisha vifo vya watu watano na wengine kujeruhiwa. =====