Zitto awaponza viongozi wa ACT Wazalendo
Jeshi la Polisi Wilayani Kigoma linawashikilia viongozi watatu wa Ngome ya Vijana Jimbo la Kigoma Mjini waliokwenda polisi kutoa taarifa ya kufanya maandamano ya amani.
Zitto Kabwe
Ngome hiyo ya vijana imeeleza kuwa mpaka sasa hakuna taarifa rasmi ya sababu gani polisi imewashikilia viongozi hao wa Vijana Kigoma Mjini huku ikidai kuwa huenda wakakosa kabisa dhamana kwa siku ya leo.
Viongozi wanaoshikiliwa na Polisi ni Said Mlindwa (Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Jimbo), Wakili Mubanga (Katibu wa Ngome ya Vijana Jimbo) na Ntakije Ntanena (Katibu Mwenezi wa Ngome ya Vijana Jimbo)
Maandamano ambayo walikuwa wameenda kuyaombea kibali ni ya amani kwaajili ya kumpongeza Mbunge wao Zitto Kabwe na madiwani kwa kazi wanayoifanya kuwaletea wananchi maendeleo.
Aidha Ngome hiyo ya Vijana imesisitiza kuwa inawaombea dhamana kwakuwa ni haki yao na wanapaswa kupewa kwa kuwa masharti ya dhamana kwa mujibu wa sheria yametimizwa.
Comments