WATANO WAGONGWA NA LORI WAKITOKA HARUSINI, WAFARIKI – VIDEO

AJALI mbaya ya lori la mchanga lenya namba za usajili T155 ATC kugongana na gari la abiria aina ya Toyota Hiace imetokea majira ya saa 8 usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Januari 5, 2019 katika maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambapo lori hilo limeacha njia na kutumbukia mtaroni.

Kutokana na taarifa ambazo hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi, inadaiwa kuwa lori hilo liliigonga Hiace ikiwa imebeba watu wengi waliyokuwa wakitoka kwenye harusi na kusababisha vifo vya watu watano na wengine kujeruhiwa.
=====

Comments

Popular posts from this blog

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL