WADAU WOTE WA ELIMU MNATANGAZIWA KUWA ,NOTES ZA MASOMO YA SAYANSI KWA VITENDO (PRRACTICAL) BIOLOGY ,PHYSICS, CHEMISTRY KWA UPANDE WA OLEVEL, ZINAPATIKANA HAPA ZINGINE PIA
Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC Na Upendo Mosha-Moshi MKUU wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Kippi Warioba, ametuhumiwa na wananchiwa Kijiji cha Chekereni Weruweru, Kata ya Kindi kuvamia na kuvunja ofisi ya kijijihicho na kuchukua nyaraka mbalimbali. Kutokanana hali hiyo wananchi hao wametishia kumfikisha mahakamani kwa madai ya kuvunja kufuli la ofisi ya kijiji na kuchukua nyaraka hizo. Mwenyekiti wa kijiji hicho, John Bosco, aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana kijijini hapo. Bosco alisema kiongozi huyo amekuwa ni sehemu ya kuchochea migogoro na kwamba hawapotayari kuchonganishwa bali watafuata sheria. Alisema mgogoro huo ulianza baada ya mkuu huyo wa wilaya, kutumia nguvu nakuwanyang’anya kijiji ofisi yake na kukipa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jambo ambalo ndio chanzo cha mgogoro huo. “Tunataka mahakama itafsiri kuwa ofisi ya Kijiji cha Chekereni Weruweru ni mali ya Serikaliya kijiji au CCM… mk...
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameziagiza kampuni zote zinazosambaza nguzo za umeme kulipa ushuru wa halmashauri wanakotoa nguzo hizo amboa ni asilimia tano ya gharama ya kila nguzo kama ilivyoelekezwa na Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Ametoa agizo hilo jana Jumatatu, Januari 7, 2019 baada ya kupata taarifa kuhusu kampuni ya New Forest ambayo inamkataba na TANESCO wa kusambaza nguzo za umeme, kukaidi kulipa ushuru wa asilimia tano ya gharama ya kila nguzo. Ushuru huo umefikia sh. bilioni 2.9 hali iliyopelekea uongozi wa mkoa kuzuia nguzo hizo zisitoke. Wiki iliyopita akiwa katika ziara ya mkoa Ruvuma, Waziri Mkuu alipokea malalamiko kuhusu mkoa wa Iringa kuzuia kusambazwa kwa nguzo za umeme ndipo alipoamua kuwaita Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi pamoja na wakuu wa wilaya, wakurugenzi pamoja na wenyeviti wa halmashauri wanaotoka katika wilaya zinazozalisha nguzo. Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni...
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameukwepa mtego wa Rais Dk. John Magufuli kuhusu hatima ya ufukwe wa Coco. Hatua hiyo inatokana na uamuzi wake wa kuanza kueleza mikakati itakayofanyika, ikiwamo kuundeleza ufukwe huo sambamba na kujenga mabanda kwa wafanyabiashara na vyoo vya kisasa. Kutokana na maelezo hayo ya utangulizi, Rais Magufuli alisema amemkwepa kwa kumuwahi kwani ilikuwa kuna uamuzi mgumu dhidi yake. Alisema ufukwe huo wa Coco unatia aibu kwa sababu hakuna hata choo hali ya kuwa mapato yanakusanywa kila siku. Mkuu huyo wa nchi alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kisasa la Selander ambalo linapita baharini. “Nimefurahi maneno ya RC (Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda) kuwa wataboresha pale Coco Beach kuliko kukaa vile kwa sababu panatia aibu kwa jiji kama la Dar es Salaam. “Eneo lile halina hata choo, ni lazima tuzizungumze aibu, lakini wanakusanya mapato kila ...
Comments