Posts

Songea kukopesha Wanawake na Vijana kukwama

on Songea yakwama kukopesha Wanawake na Vijan Manispaa ya songea mkoani Ruvuma, imeshindwa kuendelea kukopesha vikundi vya wanawake na vijana kupitia mapatoyake ya ndani, baada ya vikundi hivyo kushindwa kurejesha fedha za mikopo kwa wakati na vinadaiwa zaidi ya sh. milioni 59. Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Tina Sekambo ametoa taarifa katika kikao cha kamati ya ushauri na maendeleo ya mkoa wa Ruvuma (RCC), kuwa vikundi vilivyoshindwa kurejesha mikopo vingi vilikopeshwa katika kipindi cha mwaka 2017/18, na hadi kufika mwezi novemba 2018, na nikikundi kimoja pekee ambacho kimeweza kupunguza deni lake. Katika kipindi hicho cha miaka miwili manispaa hiyo imeweza kuwakopesha wanawake na vijana fedha kupitia makusanyo yeke ya ndani asilimia 10 kila mwezi, ambapo sh. milioni 31.10 zimekopeshwa kwa vikundi vya wanawake, na vijana sh. milioni 28.1. kwa lengo la kupambana na umasikini kwa njia ya ujasiriamali kwa kufanya kazi za mikono, ikiwemo kilimo na biashara ndogo ndogo ili waweze k...

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 2, 2019

Image
on Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 2, 2019 Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 2, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.                

Waziri Mkuu atoa ombi kwa Wananchi

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Wananchi kuendelea kushirikiana katika kuibua na kubuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maendeleo . Waziri Mkuu ameyasema hayo     wakati akipokea msaada wa vyumba viwili vya madarasa vikiwa na  madawati vyenye thamani ya sh. milioni 80 kutoka kwa bank ya CRDB, Kata ya Nachingwea Mkoani Lind i. “Nawaomba wananchi wenzangu tuendelee kushirikiana katika kuibua na kubuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maendeleo kwenye kata yetu ya Nachingwea.” alisema Majaliwa  Pia Waziri Mkuu alikabidhi kompyuta 20 kwa shule za sekondari tano ambazo ni Kassim Majaliwa, Likunja, Mnacho, Hawa Mchopa na Ruangwa.

VIDEO: Mrisho Gambo kutua na tuzo kwa Rais Magufuli

Image
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amekabidhiwa Tuzo maalum kwa ajili kwenda Rais Magufuli ambapo ni shukrani zao kwa ajili ya kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi cha miaka mtatu tangu aingie madarakani.  PATA MAARIFA ZAIDI

Fahamu faida za Kitunguu Maji mwilini mwako

Image
Kitunguu maji ni aina ya mboga yenye harufu kali inayochangamsha mwili. Pia kitunguu ni kiungo ambacho kina virutubisho katika vyakula na kuvifanya viwe na ladha nzuri. Nchi mashuhuri na maarufu inayolima kiungo hicho ni Misri na kusambaa zaidi duniani na nchini Tanzania kinalimwa zaidi katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Arusha na mikoa mingine ambayo ina rutba nzuri ya kustawisha kiungo hicho. Kiungo hicho kimekuwa kikitibu na kuponya maradhi mbalimbali kutokana na kuwa na salfa ambayo ni nzuri, hasa kwenye ini na husaidia kuponya kansa kwenye utumbo na kinywa kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya vitamini C. Kitunguu maji kina kazi nyingi katika mwili wa binaadamu, kwani hutibu magonjwa mbalimbali, ikiwemo kikohozi, vidonda vya tumbo na mifupa, ngozi koo, figo, tumbo na mkojo, kufunga hamu ya kula, hutia kiu na hulainisha tumboni. Pia, kitunguu maji ni chanzo cha madini mengi ambayo yanapatikana katika kiungo hicho ambayo yana umuhimu mkubwa ...

HABARI KUBWA MAGAZETINI LEO30/12/2018

Image
   PATA MAARIFA ZAIDI

PIGO JINGINE:Dkt. Mashinji na wenzake watatu waswekwa ndani

Image
Dkt. Mashinji na wenzake watatu waswekwa ndani Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji na viongozi wengine watatu wa chama hicho wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Hai, Mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali. Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Hai ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya ambapo amesema kuwa viongozi hao wamekamatwa mchana kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usiokuwa halali. “Ni kweli tumemkamata Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Mashinji, katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Basir Lema, mwenyekiti wa halmashauri ya Hai, Egra Mchomvu na msaidizi wa mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, Irine Lema kwa kufanya mkusanyiko usio halali,” amesema. Amesema kuwa viongozi hao, wamekutwa wakifanya mkusanyiko katika eneo la Boma bila ya kuwa na kibali jambo ambalo ni kinyume cha sheria. ...

HapoKale: Wachaga na kisa cha kurudi nyumbani kila mwisho wa mwaka

Image
  Wachaga na kisa cha kurudi nyumbani kila mwisho wa mwaka Wachaga ni kabila lenye asili ya Kibantu na mchanganyiko wa asili ya Kikushi wanaoishi kaskazini mwa Tanzania, Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro. Kabila la Wachaga linatajwa kuwa la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania, ambapo takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachaga ni watu 2,000,000. Shughuli kubwa ya Wachaga ni biashara, kilimo na kazi za ofisini. “Mangi” ni jina waliloitwa watawala wa Kichaga. Hawa walimiliki mashamba, Ng’ombe na waliheshimiwa kama viongozi wa kikabila. Mangi walikuwa na nguvu za kisiasa na utajiri. Baadhi ya Mangi mashuhuri katika historia ni Mangi Rindi aliyeingia mikataba na wakoloni (Wajerumani), Mangi Sina wa Kibosho – anajulikana kwa uhodari wake wa vita katika kupigana na Wamachame na kupora ng’ombe na mazao yao, ...

Liverpool yaipasua Arsenal, Firmino achoma kibanda cha bunduki

Image
Liverpool yaipasua Arsenal, Firmino achoma kibanda cha bunduki Klabu ya Liverpool jana imeipasua Arsenal kwa kipigo cha 5-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza, ushindi ulioiwezesha kujikita zaidi kileleni huku ikitishia usalama wa wapinzani wake. Arsenal ilikuwa ya kwanza kuchokoza nyavu za Liverpool katika dakika ya 11 baada ya Ainsley Maitland-Niles kupata upenyo na kujikita ndani ya 18 akiwaacha walinzi wa Liverpool kwa mbali. Lakini jua lililoonekana mbele ya Unai Emery halikuwa la machweo bali lilikuwa la alfajiri na kazi ilikuwa inaanza. Liverpool walijibu dakika tatu baadaye kupitia kwa Roberto Fermito aliyetumia makosa ya safu ya ulinzi ya washika bunduki hao iliyojichanganya. Hata hivyo, Fermito hakuwaacha wanywe maji kwa mshangao wa msawazisho na alipachika goli la pili katika dakika ya 16 ikiwa ni dakika mbili tu tangu ashangilie goli la kwanza. Mvua ya magoli ilianza kufunguka taratibu dhidi ya Arsenal, a...

TANZIA: Mwanasiasa mkongwe nchini afariki dunia

Image
16 hours ago Comments Off on TANZIA: Mwanasiasa mkongwe nchini afariki dunia Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Pancras Ndejembi amefariki dunia leo Jumamosi Desemba 29, 2018 majira ya saa 3:30 asubuhi. Ndejembi amefariki katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alikopelekwa kwaajili ya matibabu baada ya hali yake kubadilika ghafla. Aidha, mtoto wa Marehemu, Edna Ndejembi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, huku akisema baba yake alikuwa anasumbuliwa na kifua kubana ambapo alilazwa katika Hospitali ya DCMC ya jijini Dodoma na kuruhusiwa juzi Alhamisi akiwa ameimarika kiafya. “Lakini jana jioni hali yake ilibadilika ghafla ndipo tukamkimbiza hapo hospitali ya mkoa na leo saa tatu asubuhi mzee ametutoka,” amesema Edna. Hata hivyo, Mzee Ndejembi aliwahi kuwa mkuu wa wilaya mbalimbali nchini na baadaye akawa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa ...

MAKTABA -PAST PAPERS

MAKTABA -PAST PAPERS FORM SIX MAKTABA PAST PAPERS FORM FOUR  MAKTABA -PAST PAPERS FORM TWO MAKTABA PRIMARY

PHYSICS 2B F4-2010

PHYSICS 2B F4 -2011

PHYSICS 2B F4-2012

PHYSICS 2B F4-2013

PHYSICS 2C F4-2010

PHYSICS 2B F4-2017

PHYSICS 2B F4-2016

PHYSICS 2B F4-2015

PHYSICS 2C F4-2011