'Namshangaa sana Mungu'' - Magufuli
Jumapili , 23rd Dec , 2018 Na Fatuma Muna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amekiri kushangazwa na mambo Mungu anayoitendea Tanzania katiika kipindi hiki. Rais Magufuli akiongea wakati wa kupokea ndege. Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akihutubia katika mapokezi ya ndege aina ya 'Air Bus' A220-300 leo, Disemba 23 jijini Dar es salaam. Amesema kwamba kwa baraka ambazo Mungu amekuwa akiipatia Tanzania ni wazi haitashikika na kwamba mambo yataendelea kunyooka sana. "Nataka niwahakikishie kadiri tunavyoendelea Tanzania haitashikika tutakuwa juu mno. Tanzania tunaweza na tutaweza. Mambo yananyooka mno mpaka mimi namshangaa Mungu. Mungu anatupenda na yupo pamoja na sisi", - amesema. Pamoja na hayo, Rais Magufuli amesema kwamba 'Air Bus' ni dege ya kwanza katika nch...