JPM alivyomsifia Mufti wa Tanzania
Anna Potinus – Dar es salaam
Rais John Magufuli amempongeza Shekhe Mkuu na Mufti wa Tanzani, Aboubakar Zubeir kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake huku akidai ni mtu wa tofauti katika utendaji kazi wake.
Pongezi hizo amezitoa leo Desemba 17, 2018 katika maadhimisho ya kilele cha miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) jijini Dar es salaam.
Amesema Mufti Zuberi amesaidia kuwaleta watanzania pamoja huku akifichua siri ya utendaji kazi wake.
“Mufti wewe ni wa tofauti sana kuna siri sijawahi kuitoa lakini leo nitazungumza, wakati mzee Kikwete amepata msiba kule Msoga nilienda kumpa pole wakati wanachimba kaburi nilimuona Mufti akitoa udongo kaburini nilimuona ni mtu wa pekee maana sijawahi kumuona padre wala mchungaji akifanya hivyo na kama wapo waliowahi kuona naomba mnisamehe,”amesema.
“Sisi wa pembeni tunaweza kumuonaMufti ni wa tofauti na ninaamini katika kipindi chako cha uongzi wa miaka mitatu umewaunganisha watanzania inawezekana leo wasione lakini ukifa watasema hawajawahi kumuona Mufti kama wewe kwani haujikwezi na umetanguliza mbele maandiko na Mungu,” amesema.
Katika hafla hiyo ambayo wanasheherekea miaka hamsini ya Bakwata tangu ianzishwe Desemba 17, 1968 Rais Magufuli ametoa kiasi cha Shilingi milioni 30 huku akiwataka wazitumie watakavyo wao.
Comments