Haswa :CCM yazidi kujiimarisha


Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimemrejeshea uanachama wa chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dares Salaam, Ramadhani Madabida na wenyeviti wengine wanne baada ya kujiridhisha na maombi yao ya kutaka kusamehewa kwa makosa yao wakiwa wenyeviti wa chama hicho.
Aidha, halmashauri hiyo, imemuweka chini ya uangalizi aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, ambaye pia ameomba kurejeshewa uanachama baada ya kufukuzwa kwa makosa ya kimaadili.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumanne Desemba 18, Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, amewataja waliosamehewa pamoja na Madabida ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga, Erasto Kwirasa, Christopher Sanya (Mara) na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge.
“Hatua hiyo imefikiwa leo katika kikao cha halmashauri ya chama  kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli ambapo pamoja na mambo mengine kimepokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 ya Tanzania Bara na Zanzibar.
“Pia kikao hicho kimepokea taarifa kuhusu masuala ya maadili, kuridhia marekebisho ya kanuni mpya ya fedha na mali za chama na jumuiya zake na kuridhia uteuzi wa wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa CCM,” amesema Dk. Bashiru.

Comments

Popular posts from this blog

Wanakijiji watishia kumburuza kortini DC

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja