Waziri wa Viwanda atoa siku 14 Brela



Nora Damian, Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda, ametoa siku 14 kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), kurekebisha mifumo ya kielektroniki ya utoaji huduma za wakala huo.
Akizungumza baada ya kutembelea wakala huo leo Desemba 18, Kakunda amesema mifumo ya kielektroniki imekuwa ikilalamikiwa na watu wengi hasa katika siku za karibuni.
“Ndani ya wiki mbili nimekuja tena hapa kwa sababu kuna sababu maalumu, udhaifu mkubwa uko kwenye mifumo kuliko uhalisia.
“Kila nikipokea simu 10 za wafanyabiashara nane zinalalamikia Brela hili ni tatizo,” amesema Kakunda.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Emmanuel Kakwezi, amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama za upungufu wa watumishi 51 na mfumo kutokuwa imara.
“Kuna changamoto ya mtandao wa ORS katikati yakazi unaweza kuzimika. Mteja anatuma maombi lakini haionekani na sisi tunaweza kumjibu lakini haoni,” amesema Kakwezi.

Comments

Popular posts from this blog

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Waziri asimamisha likizo za Marubani ATCL