Posts

INATISHA! Akutwa Amekufa Kwenye Kiroba Dar – VIDEO

Image
MWILI wa mtu mmoja ambaye jina lake halijajulikana umekutwa ukiwa umefungwa kwenye kiroba na kutupwa kando ya barabara katika eneo la Karibu na Chuo cha Ustawi wa Jamii mkabala na Ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kilichopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Mtu huyo ambaye hakufahamika hata jinsia yake kutokana na namna ambavyo kiroba hicho kilikuwa kimefungwa juu na chini, anadaiwa huenda aliawa na mwili wake kutupwa ndani ya mfereji katika eneo hilo. Global TV Online imefunga safari mpaka eneo la tukio na hii ndiyo hali halisi ilivyokuwa baada ya kuukuta mwili huo huku wananchi wa eneo hilo wakihamaki kutokana na tukio hilo la kinyama.

HABARI ZA LEO ALHAMISI Januari 17, 2019

Image
Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo ALHAMISI january 17, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Abdul Nondo aja kivingine, ‘Huu muswada haufai

Image
Mwanaharakati kijana, Abdul Nondo amesema kuwa baadhi ya vifungu vilivyomo kwenye muswada wa sheria ya vyama vya siasa, vinahitaji kufanyiwa marekebisho ili kuendana na uhalisia wa demokrasia nchini. Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media mara baada ya kumalizika kwa Kongamano la kutoa maoni kuhusu muswada huo lililoandaliwa na chama cha mapinduzi (CCM), ambapo amesema vifungu hivyo vinatakiwa kutolewa ili muswada huo uweze kuimarisha demokrasia nchini. ”Muswada huu unahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa, kuna vifungu ndani yake vinatakiwa kuondolewa kabisa ili tuweze kukuza uhai wa demokrasia yetu hapa nchini,”amesema Nondo

Spika: Tumesitisha kufanya kazi na CAG

Image
MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM SPIKA wa Bunge Job Ndugai, amesema kwa sasa Bunge limesitisha kufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad. Kutokana na hali hiyo, amewatawanya wajumbe wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Tawala za Mikoa na Mitaa (LAAC) kufanya kazi katika kamati nyingine. Hatua ya usitishaji huo inatokana na kauli ya Profesa Assad aliyoitoa Desemba mwaka jana katika mahojiano na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Arnold Kayanda. Mtangazaji huyo alimuuliza CAG kuwa ni vipi ofisi yake imekuwa ikijitahidi kila mwaka kufanya ukaguzi na kutoa ripoti zenye kuonesha kuna ubadhirifu, lakini baada ya hapo wananchi hawaoni kinachoendelea. Katika majibu yake CAG alisema; “Hilo ni jambo ambalo kimsingi ni kazi ya Bunge. Kama tunatoa ripoti zinazoonyesha kuna ubadhirifu halafu hatua hazichukuliwi, huo kwangu ni udhaifu wa Bunge. “Bunge linatakiwa kus...

Kangi Lugola amtaka Musilimu kujipima, atumbua makamanda watatu

Image
Ramadhan Hassan, Dodoma Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amemtaka Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Musilimu, kujitafakari kutokana na rushwa iliyokithiri na uonevu kwa wenye magari. Kauli hiyo ameitoa leo Jumatano Januari 16, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amedai kwamba kumekuwa na utaratibu wa askari wa usalama barabarani kuwabambikizia watu kesi huku wakichukua rushwa wazi wazi bila kificho. “Askari wa barabarani wamekuwa wakiwatoza watu kwa makosa ambayo hayaeleweki, namuomba Kamanda wa Usalama Barabarani ajitafakari,” amesema. Katika hatua nyingine Waziri huyo wa Mambo ya Ndani ya Nchi amewasimamisha kazi makamanda watatu wa polisi kwa makosa mbalimbali ikiwemo kutotii maagizo yake. Makamanda waliosimamishwa kazi ni pamoja na wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala Salum Hamduni, Temeke, Emanuel Lukula na wa Arusha Ramadhan Ng’azi. “Sababu za kuwasimamisha Kamanda wa Ilala na Temeke ...

CCM yaifagilia Sheria Mabadiliko ya Vyama vya Siasa

Image
Elizabeth Joachim, Dar es Salaam Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amesema sheria vya vyama vya siasa iliyopo sasa haimpi nguvu Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya kazi kwa ufanisi hivyo mabadiliko ya muswada mpya yatasaidia uimara wa vyama vya siasa na Ofisi ya Msajili kufanya kazi kwa ufanisi. Polepole ameyasema hayo leo Jumatano Januari 16 katika mkutano wa chama hicho wa kujadili mabadiliko ya muswada kabla ya kupelekwa Bungeni uliofanyika Jijini Dar es Salaam. “Mabadiliko hayo yatampa nguvu msajili wa vyama vya siasa kutazama kwa jicho la upole endapo chama kimefanya vizuri na jicho la ukali kwa mambo ya ovyo ambayo hama kitafanya,” amesema. Aidha, amesema mabadiliko hayo yatampa nguvu Msajili kuhusika kwenye usajili wa vyama vya siasa, kusimamia chaguzi za vyama vya ndani, kutoa na kufuatilia uwajibikaji wa ruzuku. “Sheria tunayoitumia sasa ni sheria ya mwaka 2010 ni miaka 10 imepita tangu kufanya mabadiliko ya s...

SOMA HIYOO! Magaidi walioshambulia hoteli Nairobi wafanyiwa hivi

Image
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema kuwa magaidi waliohusika kufanya shambulio la kuvamia hoteli la kifahari ya DusitD2 iliyopo nchini Kenya jijini Nairobi tayari wameuawa na operesheni imekamilika. Hata hivyo shambulio hilo limeleta madhara makubwa ikiwemo kusababisha vifo vya watu 14 pamoja na majeruhi huku wengine 700 wakiwa wamefanikiwa kuokolewa katika janga hilo lililoikumba nchi ya Kenya siku ya jana. Ambapo kundi la kigaidi la Al-shabaab limekiri kuhusika na shambulio hilo ambapo jana majira ya saa 9 jioni walivamia hoteli hiyo na kufanya shambulio hilo katika eneo la 14 Riverside. Shambulio hilo la kigaidi lililotajwa kufanywa na watu sita lililohusisha milio ya risasi pamoja na mabomu yaliyotawala na kusababisha vurugu kubwa katika eneo hilo. Aidha hali ya sasa ni shwari mara baada ya jeshi la polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama kumaliza operesheni hiyo ya kufanya jiji litulie na kuwa na amani baada ya mtikisiko huo.

LIVE: Rais Magufuli akipokea hati za utambulisho wa Mabalozi

Image
Fuatilia hapa moja kwa moja kutoka Ikulu jijini Dar es salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho wa mabalozi mbalimbali leo Januari 16, 2019

HABARI ZA LEO JUMATANO 16/1/2019

Image