Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 9, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani
AZIZA MASOUD – Dar es Salaam MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema, amesema hawezi kuungana na vyama vingine vya upinzani vilivyofungua kesi kupinga Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018. Amesema anaamini kufanya hivyo hakuwezi kuondoa matatizo yaliyopo ambayo msingi wake unatokana na ubovu wa sheria zilizopo. Mrema ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja kupita baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuanza kusikiliza kesi namba 31 ya kupinga muswada huo iliyofunguliwa mahakamani hapo Desemba 20 mwaka jana na viongozi wa vyama vya upinzani. Viongozi hao ni Kiongozi Mkuu ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, Kaimu Katibu Mkuu Cuf (Bara), Joram Bashange na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa chama hicho, Salim Bimani. Katika kesi hiyo mshtakiwa mkuu ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Adelardus Kilangi. Akizungumza na waandishi wa habari jana nyumbani kwake Salasala, Dar es Salaam, Mrema alisema wapinzani wanapaswa kufahamu kuwa hitaji la sasa...
KAMISHNA Mkuu Wa Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Siyanga, amesema uchunguzi waliyoufanyika wamebaini kuwa mwili wa mfanyabiashara, Happy Mboya (38) aliyefariki dunia katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam haukuwa na dawa za kulevya kama ilivyoripotiwa awali. Happy aliyefariki dunia Jumapili iliyopita Desemba 16, 2018 na mwili wake kupangwa kusafirishwa jana kwenda Moshi kwa mazishi, Polisi wa Kituo cha Oysterbay waliuchukua kwa ajili kuupeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi baada ya kudaiwa kuwa ulikuwa na madawa ya kulevya tumboni. Siyanga amesema maofisa wa Mamlaka hiyo walikuwepo wakati mwili wa marehemu Happy ukifanyiwa upasuaji na haukukutwa na dawa za kulevya kama ilivyodaiwa. Jana Siyanga alisema baada ya uchunguzi huo angetoa taarifa kamili juu ya tukio hilo. Baba mdogo wa marehemu, Ally Bilali jana alisema baada ya kurejea nchini, Happy alifikia katika nyumba ya kulala wageni ambayo haik...
Na Kulwa Mzee-DAR ES SALAAM MFANYABIASHARA Akram Azizi aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka 75 ya uhujumu uchumi ikiwamo ya kukutwa na nyara za Serikali, silaha 70, risasi 6,496 na kutakatisha Dola 9,018 za Marekani, amefutiwa mashtaka baada ya kulipa faini ya Sh milioni 259. Akramu alifutiwa mashtaka hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kufunguliwa upya mashtaka 73 yakiwamo ya kukutwa na silaha bila kibali, kukutwa na risasi na kilo tano za nyama ya nyati. Mashtaka mapya yalisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi, akisaidiana na Wakili Simon Wankyo. Katika mashtaka 75 yaliyofutwa anadaiwa kuyatenda makosa hayo kati ya Juni na Oktoba 30 na 31, mwaka huu katika maeneo ya Oysterbay. Katika shtaka la kwanza anadaiwa Oktoba 30, mwaka huu maeneo ya Oysterbay alikutwa na meno sita ya tembo yenye thamani ya Sh 103,095,000. Shtaka la pili anadaiwa Oktoba 30, mwaka huu alikutwa na kilo 65 ya ny...
Comments