Sakata la Korosho laibuka Bungeni, Serikali yatoa majibu
Sakata la bei ya korosho laibuliwa bungeni mara baada ya kuwepo taarifa za kununuliwa zao hilo chini ya bei elekezi ya Tsh. 3,300 kwa kilo. Naibu Waziri wa kilimo, Omar Mgumba amesema kuwa Korosho hununuliwa kwa bei ya 3,300 kama alivyoelekeza Rais Magufuli na bei hiyo haijakiukwa. Hata hivyo ameeleza kuwa bei ya Tsh. 3,300 kwa korosha daraja la kwanza, huku daraja la pili ikinunuliwa kwa Tsh. 2,640. "Hadi kufikia January 30, 2019 Serikali imenunua jumla ya tani 214,269.684 za korosho ghafi zenye thamani ya Sh. 707,089,957,200.00 sawa na asilimia 89.3 ya lengo la uzalishaji," amesema. Aliendelea kwa kueleza kuwa jumla ya wakulima 390,466 wamekwisha lipwa hadi kufikia January 30 mwaka huu, huku Vyama vya msingi 603 vimelipwa kati ya vyama vya msingi 605 vilivyohakikiwa. Utakumbuka awali Mbuge wa Mchinga kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Awali Bobali alisema kuwa korosho imekuwa ikinunuliwa kwa bei ya Tsh. 2,640 kwa kilo na yupo tayari kujiuzulu iwapo ni kwel...