JPM afichua akaunti 3,000 feki za korosho
AZIZA MASOUD-DAR ES SALAAM RAIS Dk. John Magufuli, amesema kuna wafanyabiashara 3,000 walifungua akaunti feki ili walipwe fedha za korosho. Pia amesema wanaolalamikia fedha za ununuzi wa korosho ni wafanyabiashara wasiokuwa na mashamba na amesisitiza Serikali haitawalipa watu hao kwa kuwa hawana uhalali wa kupata malipo hayo. Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana aposhuhudia utiaji saini wa mkataba wa kuuziana tani 36,000 za mahindi zenye thamani ya Sh bilioni 21 kati ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP). “Ununuzi wa korosho unaenda vizuri, wanaopiga kelele ni wale makambonga kwa sababu walinunua korosho walifikiri watalipwa fedha, wanapoulizwa mashamba yako wapi hawayaonyeshi kwa hiyo hawalipwi, wale ndio wanapiga kelele na tumeshajua kuna akaunti karibu 3,000 feki watu walizifungua nazo hazilipwi,” alisema. Magufuli alisema Serikali haina shida na wafanyabiashara isipokuwa inahitaji watu wanaof