Mdee:viongozi bora CCM 2018
Mbunge wa Kawe kupitia kiti cha Chadema ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (BAWACHA), Halima Mdee kuelekea kuufunga mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka 2019 amezungumzia viongozi wachache wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Rais John Pombe Magufuli waliofanya vizuri katika kuwatumikia wananchi kwa mwaka 2018 katika serikali ya awamu ya tano.
Kwenye orodha hiyo amewataja; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi na Katibu Mkuu (TAMISEMI), Eng. Mussa Iyombe.
”Kidunchu sana naweza nikamtaja Katibu Mkuu wa Tamisemi, Iyombe yeye alijaribu kutuliza ‘temperature’ sababu alitoa ‘statement’ ambayo ni ya adimu sana kuisikia katika awamu hii”, Mdee.
”Jafo naye kidogo katika mawaziri wote ameonesha utofauti wa kuzungumza kile ambacho wengi wameogopa kuzungumza”, Mdee.
”Lukuvi naye kidogo ameonesha jitihada kwa kiwango fulani kwa utatuzi wa migogoro ya ardhi amafanyia kazi kwa kiwango kidogo maoni ya kambi rasmi ya upinzani ya masuala ya ardhi”, Mdee.
Aidha, kumekuwa na tabia ya viongozi wa upinzani kotokukubaliana na kile kinachofanywa na viongozi wa Chama tawala CCM, hivyo Mdee amezungumza hayo siku chache zilizopita
Comments