Popular posts from this blog
Wapinzani: Spika tengua kauli yako
By
Maguruacademy
-
SARAH MOSES -DODOMA KAMBI ya Upinzani Bungeni, imemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai, kutengua uamuzi wake wa kusimamisha vikao vya kamati za Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa ( LAAC ). Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma jana, Mwakilishi wa Kambi ya Upinzani, John Mnyika alisema kauli aliyoitoa spika siyo ya Bunge, bali ni yake binafsi. “Haiwezekani mgogoro wa Spika na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Musa Assad, ukasimamisha mambo mengine ya bunge kuendelea. “Kama kamati tunamtaka spika abadilishe uamuzi wake kwa kamati hizi mbili na awezeshe kamati hizo kukutana kabla ya tarehe 25 mwezi huu,”alisema Mnyika na kuongeza: “Tumesikia spika amesimamisha kamati hizo kwa kuwa CAG ameitwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Januari 21, mwaka huu kwa kile alichokiita mgogoro wa CAG na Bunge … kauli hiyo siyo ya Bunge ila ni yake binafsi”. Alisema uamuzi alioutangaza Spika
Kitakachojiri katika mabasi Des. 20
By
Maguruacademy
-
LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM MABASI ya abiria yanayofanya safari kwenda mikoani na nchi jirani, yanatarajia kuanza safari saa 11:00 alfajiri katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki Mabasi Tanzania (Taboa), Enea Mrutu aliliambia MTANZANIA jana kuwa hatua hiyo ilifikiwa katika kikao kati yao, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani. Mrutu alisema utaratibu huo utayahusu mabasi yanayokwenda mikoa yote nchini isipokuwa katika maeneo yenye changamoto kubwaya kiusalama ikiwamo Kigoma, Sumbawanga na Rukwa. Alisema utaratibu huo utaanza kutekelezwa Desemba 20 mwaka huu, ambapo magari yote yaliyokuwa yakizuiwa Dodoma, Morogoro na Shinyanga sasa yataruhusiwa kutembea usiku ili yakamilishe safari. “Kwa mfano njia ya kati sehemu yenye changamoto ni kutoka Shinyanga kwenda Mwanza, hapo tumekubaliana uwekwe utaratibu kwamba kwa sababu magari ni meng
Comments