Mahakama ya DR Congo yaidhinisha ushindi wa Felix Tshisekedi, Fayulu aitisha maandamano
Mahakama ya katiba DR Congo imemuidhinisha rasmi Felix Tshisekedi kuwa rais wa nchi hiyo. Mgombea aliyechukua nafasi ya pili katika matokeo ya uchaguzi wa urais nchini DR Congo Martin Fayulu ameitaka jamii ya kimataifa kutotambua matokeo hayo na ameitisha maandamano. Taarifa yake inajiri baada ya ya mahakama ya kikatiba kuidhinisha ushindi wa mgombea mwengine wa upinzani , Felix Tshisekedi . Muungano wa Afrika ulisema siku ya Ijumaa kwamba kulikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu matokeo hayo na kutaka matokeo rasmi kucheleweshwa. Bwana fayulu sio mgombea pekee ambaye anaamini kwamba yeye ni muathiriwa wa wizi wa kura huku data ilioibwa ikionyesha kuwa alipata kura mara tatu ya kura alizopata Tshisekedi. Haijulikani iwapo raia wataheshimu wito wa Fayulu wa kufanya maandamano. Siku ya Jumatatu ujumbe wa AU unatarajiwa Kinshasa na unatarajiwa kukutana na mtu anayedaiwa 'kuiba' kura rais anayeondoka madarakani Joseph Kabila. Iwapo Tshisekedi ataapishwa , muungano ...