Mlezi wa timu ya taifa ya soka ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, amewapongeza wachezaji hao kwa ubingwa wa COSAFA walioutwaa nchini Botswana. Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi akipokea kombe la COSAFA kutoka kwa nahodha wa Serengeti Boys Michael Morris. Dkt. Mengi ametoa pongezi hizo leo Desemba 20, 2018 katika hafla ya chakula cha mchana alioyowaandalia vijana hao pamoja na viongozi wa TFF na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Waziri Harrison Mwakyembe. Akiongea katika hafla hiyo Dkt. Mengi amesema, ''nyinyi mlizaliwa washindi na siku zote nalisema hilo, nawashukuru vijana wangu kwa kutekeleza ahadi ya kurudi na kombe hili kama mlezi wenu nimejisikia vizuri sana'', amesema. Katika hafla ya ch...
Comments