Posts

DRC CONGO :UN YAVIMBIWA

Image
Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Corneille Nangaa, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia mawasiliano ya Satellite kuwa Congo ina njia mbili za kukubali matokeo hayo au kuyafuta. Amesema kuwa iwapo matokeo yatafutwa, nchi haitakuwa na rais mpya mpaka uchaguzi mwingine utakapo anadaliwa. Aidha, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa kiti cha urais, ambapo Felix Tshisekedi aliibuka kidedea, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana New York Ijumaa kuzungumzia uchaguzi huo. Rais aliyeko madarakani, Joseph Kabila tayari ameendelea kutawala kwa zaidi ya miaka miwili baada ya muhula wake kumalizika, na alikuwa tayari amejitayarisha kuachia madaraka mwezi huu mara tu rais mpya atakapo chaguliwa. Hata hivyo, katika uchaguzi huo, Kabila alimuunga mkono waziri wake wa mambo ya ndani wa zamani, Emmanuel Shadary, ambaye alichukuwa nafasi ya tatu, huku wafuasi wa Fayulu wakimtuhumu Kabila kwa kufanya makubaliano na...

HABARI ZA LEO JUMAMOSI 12/1/2019

Image

KESI YA ZITTO MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA YAHAMISHWA

Image
KESI ya Kiongozi wa ACT Wazalendo na wenzake wa vyama 10 vya upinzani ya kupinga muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa iliyopangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu leo majira ya saa 3 asubuhi, limehamishiwa kwa Jaji mmoja. Shauri la kesi hiyo lilipangwa kusikilizwa na Majaji; Barke Sehel (kiongozi wa jopo), Benhajo Masoud na Salma Maghimbi, lakini limekwama baada ya wajibu maombi (Serikali) kuwasilisha pingamizi la awali wakiitaka Mahakama hiyo ilitupilie mbali. Aidha, kutokana na pingamizi hilo, Mahakama imesitisha usikilizwaji wa shauri la msingi na badala yake imeamua kuanza kusikiliza pingamizi ambapo imepanga kusikiliza pingamizi hilo na jaji Masoud katika chemba kuanzia saa 4:00, asubuhi. Zitto na Viongozi wa Upinzani kwenye Kesi Yao Mahakama Kuu Leo

MUGABE AIBIWA MKOBA WADOLA

Image
WATU watatu wamefikishwa mahakamani nchini Zimbabwe, wakishtakiwa kuiba mkoba uliokuwa na Dola za Marekani 150,000 (Sh. milioni 345) taslimu mali ya rais wa zamani wa taifa hilo, Robert Mugabe. Washukiwa hao wa wizi wanadaiwa kutumia pesa hizo kununua magari, nyumba na mifugo. Jamaa wa rais huyo wa zamani, Constantia Mugabe, ni miongoni mwa walioshtakiwa, kwa mujibu wa taarifa katika vyombo vya habari vya serikali. Mwanamke huyo anadaiwa kuwa na funguo za nyumba ya kijijini ya Mugabe iliyo eneo la Zvimba karibu na mji mkuu wa Harare, na ndiye aliyewasaidia hao wengine kuingia humo na kufika ulikokuwa mkoba huo. Washukiwa hao wengine walikuwa wameajiriwa kama wafanyakazi wa kufagia na kusafisha nyumbani humo wakati wa kutekelezwa kwa wizi huo siku moja kati ya tarehe 1 Desemba na mapema Januari mwaka huu. “Johanne Mapurisa alinunua gari aina ya Toyota Camry… na nyumba ya $20,000 baada ya kisa hicho,” mwendesha mashtaka wa serikali Teveraishe Zinyemba aliambia ...

HABARI ZALEO 11/1/2019

Image
PATA FAIDA ZAIDI HAPA