TAHARUKI: KANISA KATOLIKI LAANIKA HADHARANI JINA LA MSHINDI WA URAIS CONGO
Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (Cenco), lenye ushawishi mkubwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limesema linafahamu aliyeshinda uchaguzi wa rais ambao ulifanyika Desemba 30 mwaka jana na kuomba Tume ya Uchaguzi (CENI) kutangaza matokeo katika mazingira huru, haki na ukweli. Baraza hilo limetoa baada ya tume ya uchaguzi kutangaza kwamba italazimika kuchelewa kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita kutokana na hitilafu za kimitambo. Kanisa hilo limesema sampuli ya wawakilishi ilichapishwa katika vituo vya kupigia kura ambavyo vinawaruhusu kujua jina la rais aliyechaguliwa. Sampuli hiyo ni ya vituo zaidi ya 23,000 kati ya vituo 70,000 vilivyowekwa na Ceni nchini humo. Akizungumza na vyombo vya habari nchini humo, msemaji wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki, Padri Donatien Nshole, amesema si jukumu lao kutangaza matokeo, bali wao ni waangalizi lakini wanafahamu nani aliyechaguliwa na wananchi. “Ni muhimu kusisitiza kuwa k...