AJIUA , AMWACHIA MWANAYE BAISKELI !
B UKOBA: Salvatory Rweyemamu (47) ni baba aliyekuwa mkazi wa Kashai Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ambaye anadaiwa kujiua kwa kujinyonga kwa kile kilichodaiwa ni hali ngumu ya maisha na kusumbuliwa na ugonjwa kisha kumwachia mwanaye baiskeli kama urithi. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Rweyemamu aligundulika kuwa amefariki dunia kwenye chumba chake alichokuwa akiishi katika nyumba ya mwanamke aliyetajwa kwa jina la Tausi Ally. Ilielezwa kuwa, mwili wa Rweyemamu uligundulika Januari 6, mwaka huu, majira ya saa 3:00 asubuhi baada ya mtoto wa kaka yake kwenda kumjulia hali. Habari kutoka eneo hilo la tukio zilidai kwamba, mara baada ya kijana huyo kufika nyumbani kwa marehemu Rweyemamu alibisha hodi kwa muda mrefu bila kujibiwa. Ilielezwa kuwa, baada ya kuona hali hiyo, kijana huyo ilibidi aulizie kwa majirani ndipo majirani hao na rafiki wa marehemu, Andrew John walipochungulia kwa dirishani na kugundua mwili wa Rw...