Posts

Showing posts from February, 2019

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA ZA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA ZA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI 27 February 2019 Tangazo la Ajira Tangazo_Ajira_Mpya_Walimu_Feb2019.pdf Kuomba ajira bofya hapa http://ajira.tamisemi.go.tz

Sakata la Korosho laibuka Bungeni, Serikali yatoa majibu

Image
Sakata la bei ya korosho laibuliwa bungeni mara baada ya kuwepo taarifa za kununuliwa zao hilo chini ya bei elekezi ya Tsh. 3,300 kwa kilo. Naibu Waziri wa kilimo, Omar Mgumba amesema kuwa Korosho hununuliwa kwa bei ya 3,300 kama alivyoelekeza Rais Magufuli na bei hiyo haijakiukwa. Hata hivyo ameeleza kuwa bei ya Tsh. 3,300 kwa korosha daraja la kwanza, huku daraja la pili ikinunuliwa kwa Tsh. 2,640. "Hadi kufikia January 30, 2019 Serikali imenunua jumla ya tani 214,269.684 za korosho ghafi zenye thamani ya Sh. 707,089,957,200.00 sawa na asilimia 89.3 ya lengo la uzalishaji," amesema. Aliendelea kwa kueleza kuwa jumla ya wakulima 390,466 wamekwisha lipwa  hadi kufikia January 30 mwaka huu, huku Vyama vya msingi 603 vimelipwa kati ya vyama vya msingi 605 vilivyohakikiwa. Utakumbuka awali Mbuge wa Mchinga kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Awali Bobali alisema kuwa korosho imekuwa ikinunuliwa kwa bei ya Tsh. 2,640 kwa kilo na yupo tayari kujiuzulu iwapo ni kwel...

Ubelgji yakubali kumpa hifadi Gbagbo

Image
BLUSSELS,Ubelgji SERIKALI ya hapa imekubali kumpa hifadhi kiongozi wa zamani wa Ivory  Coast, Laurent Gbagbo, wakati akisubiri matokeo ya rufaa iliyokatwa kupinga kuachiwa na Mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia Makosa ya Uhalifu wa Kivita ICC iliyopo mjini  The Hague nchini Uholanzi. Hatua hiyo imekuja baada ya Januari 15 mwaka huu Mahakama hiyo kumwachia  Gbagbo na msaidizi wake,  Charles Ble Goude,baada ya kuwafutia mashtaka ya kuhusika na ghasia zilizolipuka katika taifa hilo la magharibi mwa Afrika mwaka  2010. Baada ya kufikia uamuzi huo, kesho yake mahakama hiyo ikaeleza kuwa haioni sababu ya kuendelea kumshikilia mahabusu na hivyo ikasema kuwa inaweza kumkabidhi kwa nchi ambayo itakuwa tayari kumpokea. “Kulikuwa na ombi kutoka mahakamani la kumpa hifadhi  Gbagbo na hiyo ilikuwa kazi rahisi kwa sababu ana familia nchini Ubelgji kwani mkewe na wanawe wanaishi Brussels,” Waziri wa Mambo ya Nje wa hapa,  Didier Reynders aliki...